Kundi la mwisho la wanajeshi wa Marekani laondoka Iraq
18 Desemba 2011Matangazo
Inakadiriwa magari 110 yaliwasafirisha askari hao, wengi wao wakiwa kutoka kikosi cha tatu na kundi la kwanza la askari wa farasi ambao walivuka mpaka majira ya saa 1:30 asubuhi. Hatua hiyo inafanya Iraq ibakiwe na askari kiasi cha mamia hivi katika ofisi za ubalozi wa Marekani. Iraq wakati mmoja iliwahi kuwa na karibu wanajeshi 170,000 wa Kimarekani katika kambi zipatazo 505. Kuondoka huko kunahitimisha mzozo na uvamizi wa kijeshi ambao ulianza kwa makombora kuushambulia mji wa Baghdad na kumalizikia kwa machafuko ya Iraq na mfumo wa demokrasia unaolegalega.
Mwandishi: Sudi Mnette