Kundi la IS lajilimbikizia silaha za sumu
11 Novemba 2016.Kaburi la pamoja lenye miili ya zaidi ya watu 100 limegundulikana katika mji wa Hammam al-Alil mojawapo ya ngome zinazotumiwa na kundi hilo linalojiita Dola la Kiislamu kufanya mauaji.Msemaji wa Umoja wa Mataifa Ravina Shamdasani amesema akizingatia ushahidi kutoka duru mbali mbali ukiwemo wa mwanaume moja aliye nusurika katika mauaji ya takriban wanajeshi 50 wa zamani wa Iraq aliejifanya amekufa.
Shamsadani amewaambia waandishi wa habari kwamba kuna sehemu nyengine nyingi zinazotumiwa kufanyia mauaji na pia kwamba wana repoti za kuwepo kwa makaburi mengine ya pamoja ambazo bado hawazikuyakinisha maeneo hayo ni pamoja na uwanja wa ndege wa Mosul na kijiji cha Tal al-Thahab.
Vikosi vya Iraq vimegunduwa mrundiko wa kemikali ya sulphur na kwamba kuna repoti za kuaminika kwamba kundi hilo limetumia vifaa vya kemikali hiyo huko Qayyara karibu na Mosul na kwamba kuna mashimo ya kemikali hiyo karibu na maeneo wanakoishi raia.
Raia arobaini wauwawa
Amesema raia arobani inaropitiwa kuuwawa hao Jumanne kwa makosa ya uhaini na kutowa ushirikiano wao kwa vikosi ya serikali ya Iraq na miili yao ilinin'ginizwa kwenye nguzo za umeme katika mji huo wa Mosul.
Kundi hilo la Dola la Kiislamu limewaweka wale wanaowaita watoto wa khalifa wakimaanisha dola la Kiislam wakiwa wamevaa vililipuzi katika mitaa ya Mosul na Umoja wa Mataifa ina repoti ambazo hazikuthibitishwa kwamba kuna wavulana na vijana wadogo miongoni mwao.
Vikosi maalum vya Iraq Ijumaa vimekuwa katika mapambano na kundi hilo la Dola la Kiislamu katika mitaa ya Mosul.Meja Generali Thamer al Hussein ni kamanda wa kikosi hicho maalum.
Amesema "Masaa 24 yaliyopita kikosi hiki kiliteka kiwanda cha saruji cha Mosul pamoja na maeneo na vijiji vilioko karibu kikiwemo kijiji cha Karama na Arej.Tunamshukuru Mungu matokeo ni mazuri.Tumewauwa zaidi ya wanamgambo aroabaini wa kundi hilo la Daesh na wanajeshi wana morali kubwa mashambulizi yetu yameandaliwa vyema na mkuu wa majeshi ya muungano."
Mapambano ya kuukombowa mji wa Mosul hivi sasa yako katika wiki yake ya nne na wakati wanajeshi wameingia katika eneo hilo lililojengewa ngome bado kuna mawiki kadhaa kama sio miezi ya kuendelea kwa mapambano.
Mwandishi : Mohamed Dahman /AFP
Mhariri: Yusuf Saumu