Kuna mauaji ya kutisha CAR - Umoja wa Mataifa
31 Mei 2017Matangazo
Umoja wa Mataifa umesema uhalifu wa kutisha katika muda wa miaka 12 kati ya mwaka 2003 na 2015 umefanywa na jeshi, makundi yenye silaha na majeshi ya kimataifa.
Ripoti hiyo, ambayo inaorodhesha pia visa vya bakaji, utumwa wa kingono, kuchoma moto kijiji kizima na hata mauaji ya kimbari yanayoweza kulingana na ya kimbari, ilitayarishwa kwa ajili ya mahakama mpya ambayo itaanzishwa mjini Bangui kuhukumu wahalifu.
Katika ripoti nyengine ya Umoja wa Mataifa, inaarifiwa kuwa ghasia zinazoongezeka nchini humo zimesababisha vifo vya mamia ya watu pamoja na kuwalazimisha raia 88,000 kuyakimbia makaazi yao tangu mwanzoni mwa mwezi huu. Idadi hiyo inawafanya watu waliokimbia makaazi yao ndani ya nchi hiyo kufikia watu 500,000.