Kumalizika maonyesho ya Berlin ya mashindano ya filamu za sinema
22 Februari 2010"Bal" ilikuwa ndio filamu ilioshinda. Filamu hiyo ya wastani ilikuwa ni mchango wa kutokea Uturuki, na ni kati ya filamu nne au tano zilizokuwa bora. Ni filamu ilioendeleza mtindo ulioonekana katika mashindano ya Filamu ya Berlin mnamo miaka ya hivi karibuni, hasa zilipata tunzo filamu kutoka mataifa yasiojulikana sana katika shughuli za sinema na pia watengenezaji wa filamu walio sio maarufu sana katika ulimwengu wa filamu. Mtengenezaji filamu wa Kituruki, Semih Kaplanoglu, sio mtu asiyejulikana; filamu yake kwa jina la "SUT" hivi sasa inaonyeshwa katika majumba ya sinema ya hapa Ujerumani. Tunzo alilopewa Kaplanoglu linawakilisha usanii uliojipatia sinema za Uturuki katika miaka iliopita.
Pia jopo la waamuzi katika sherehe za mwaka huu za mashindano ya filamu huko Berlin, chini ya rais wao, Werner Herzog,lilichagua filamu na kuzitunza. Ile filamu ya Bär ya Roman Polanski ilistahiki kushinda namna ilivotengenezwa; na pongezi iliotolewa kwa filamu hiyo ilikuwa sio tu inaelekezwa kwa mtengenezaji wake ambaye sasa yuko rumande huko Uswissi. Ile filamu ya jina la Ghost Writer ilikuwa ya kusisimua, lakini maelezo yake yalikuwa ya ufundi mkubwa na kuchezwa vizuri, kukiweko sura nzuri kulikofanyika filamu hiyo.
Tunzo kubwa ya jopo la waamuzi ilikwenda kwa mchango wa filamu ya kutokea Rumania, na zawadi ya usimulizi iliienda kwa filamu ya Kichina iliofungua maonyesho hayo. Huo ulikuwa uamuzi mzuri ambao ulidhihirisha namna jopo lilivyo na ujuzi wa kazi yake. Hali hiyo haijawa hivyo kila wakati katika siku za nyuma. Wakati huo uamuzi wa wahakiki na jopo la kimataifa nadra ulikuwa wa namna moja. Tamko moja la kulaumu: ile filamu ya kutoka Iran, kwa jina " wakati wa hasira" ilistahiki kupewa zawadi, sio tu kutokana na uwazi wake wa kisiasa. Ukiacha jambo hilo, heko yafaa lipewe jopo la mahakimu.
Jee yote yalikuwa mambo mazuri, na jua kuwaka katika sherehe za 60 za mashindano ya filamu huko Berlin? Hata kidogo. Washindi wenye kuheshimika hawajaweza kuficha kiwango kibaya cha mashindano ya mwaka huu. Na huo, kwa bahati mbaya, ndio mtindo ulioonekana miaka iliopita na ambao umeendelea katika mwaka huu wa 2010. Msingi wa mashindano hayo ya Berlin lazima ufanyiwe marekebisho ya haraka. Alama zilizo wazi zinaonekana kutokana na kwenda chini kwa kiwango cha mashindano hayo. Watengenezaji wakubwa wa filamu za sinema na filamu zilizo bora kabisa zinakwenda katika mashindano ya filamu ya huko Cannes., Ufaransa. Wote hao wanaona bora waonyeshe kazi zao mpya huko kuliko Berlin.
Lakini sasa mtu anaweza akahoji kwamba maonyesho hayo ya Berlin yana mtazamo mwengine; kwamba hapo mtu anaangaza kutokea maeneo ya mbali ya dunia, hapo ndipo watengenezaji filamu wasiokuwa maarufu wanagunduliwa. Lakini kile ambacho mwaka huu, kwa sehemu, kilichoonekana, si cha heshima ukitilia maanani juhudi zinazotakiwa zichukuliwe katika sherehe za mashindano ya kimataifa.
Sherehe hizi za mashindano ya filamu ya Berlin ni zenye kupigiwa upatu sana, zikiwa na sehemu nyingine za programu na pembeni kuwa na matamasha mengine. Lakini ikiwa uzito utawekwa zaidi kidogo katika uzuri wa filamu, kupunguza matamasha maalumu ya pembezoni mwa sherehe hiyo, na kuonesha tu zile filamu zilizo nzuri kabisa, basi hapo kutasaidia ushindani unaotakiwa. Maonyesho hayo ya Berlin bado yanaweza kubakia kuwa sherehe kubwa ya umma. Wakaazi wa Berlin wanakwenda kwa makundi katika karibu maonyesho yote, wanahoji watengenezaji wa filamu. Lakini kuna ubaya gani kuzionyesha filamu chache katika maonyesho yalio mengi? Kwa hivyo, kinachotakiwa ni ujasiri wa kuwa na filamu chache na ujasiri wa kuwa na filamu zilizo bora.
Mwandishi: Kürten, Jochen/Miraji Othman/ZR
Mhariri: Mohammed Abdulrahman