Kukiri Iran kuidungua ndege ya Ukraine kwazusha maswali
12 Januari 2020Wakati jeshi lake la anga lilikiri na kuchukua jukumu, kamanda mmoja pia alidai kuwa jeshi hilo lilionya serikali ya Tehran kufunga anga ya nchi hiyo kutokana na hofu ya Marekani kulipiza kisasi kutokana na Iran kushambulia kwa makombora vituo vya kijeshi vilivyo na wanajeshi wa Marekani nchini Iraq.
Kamanda huyo huyo pia amesema alieleza uwezekano huo kwa wakubwa wake kuwa jeshi lake limeidungua ndege hiyo mapema asubuhi ya Jumatano.
Hata hivyo , wachunguzi wa ajali ya ndege wa Iran , maafisa wa serikali na wanadiplomasia wote walikana kwa siku kadhaa baadaye kuwa kombora liliiangusha ndege hiyo chapa Boeing 737 inayoendeshwa na shirika la ndege la kimataifa la Ukraine nje ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Imam Khomenei mjini Tehran.
"Hakukuwa na kombora lililorushwa katika eneo hilo katika wakati huo," amesema Hamid Baeidinejad , balozi wa Iran nchini Uingereza, katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Sky siku ya Ijumaa, akiyaita maswali mengine juu ya madai hayo kuwa "hayakubaliki kabisa."
Kisha hadithi ikabadilika mapema asubuhi ya Jumamosi, ambapo mkuu wa jeshi la Iran akisema ndege hiyo "imelengwa bila kukusudiwa kutokana na makosa ya kibinadamu."
Iran yakiri kuidungua ndege ya Ukraine
Baeidinejad baadaye aliomba radhi katika ukurasa wa Twitter.
"Katika taarifa yangu jana katika chombo cha bahari nchini Uingereza, nilitoa matokeo rasmi ya uchunguzi yaliyotolewa na maafisa wenye dhamana nchini mwangu kuwa kombora halingeweza kufyatuliwa na kuipiga ndege ya Ukraine katika kipindi hicho," aliandika . " Nasikitika kwa kutoa taarifa ambazo si sahihi."
Lakini hata katika kukiri kuidungua ndege hiyo, madai ya taarifa ya jeshi na kikosi cha ulinzi , inazusha maswali ya nani alifahamu kuhusu shambulio hilo katika wakati gani.
Jenerali Amir Ali Hajizadeh wa mpango wa ulinzi wa anga amesema aliwaambia wakubwa wake siku ya Jumatano kuwa "tukio lililotokea kwa pamoja la kufyatuliwa kwa makombora na kuanguka kwa ndege kunaleta shaka."
Wakubwa wa Hajizadeh atakuwa kamanda wa juu , jenerali Hossein Salami. Kwa kawaida kikosi cha ulinzi wa anga kinawajibika moja kwa moja kwa kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ambaye ni siku ya Jumamosi ndipo alipokiri shambulio hilo la kombora, akielezea kuhusu ripoti ya majeshi ya nchi hiyo.
Hata hivyo taarifa ya jeshji binafsi inazusha maswali , wakati iliposema ndege hiyo ilipita "karibu mno na eneo nyeti la jeshi" linalomilikiwa na jeshi hilo la ulinzi wa anga.
Viongozi wa kidini wanahatarisha kutumbukia katika mzozo wa uhalali wakati hasira miongoni mwa wananchi wake ikitokota kutokana na jinsi taifa hilo lilivyoishughulikia taarifa ya kuanguka kwa ndege, ambapo jeshi limechukua siku tatu kukiri sababu zilizosababisha kuanguka kwake, ikiwa ni kutokana na kombora lililofyatuliwa kimakosa.