1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mali kinderarbeit

Sekione Kitojo5 Oktoba 2009

Mtoto hapaswi kufanyakazi, ambayo inaweza kuathiri mwili ama akili yake. Mtoto hapaswi kutumika kinyume na sheria kama nguvukazi rahisi.

https://p.dw.com/p/JyPQ
Mtaa mkuu katika mji mkuu wa Mali Bamako.Picha: AP

Mtoto hapaswi kufanyakazi, ambayo inaweza kuathiri mwili ama akili yake. Mtoto hapaswi kutumika kinyume na sheria kama nguvukazi rahisi.Mkataba wa umoja wa mataifa wa kuwalinda watoto unakataza hilo, pamoja na mikataba kadha ya kimataifa.

Katika nchi nyingi duniani watoto kufanyishwa kazi ni jambo la kawaida. Si wazazi ama watoto wenyewe wenye matatizo na hilo, kwasababu pamoja na hayo umasikini unawafanya wasiwe na la kuchagua. Mfano ni katika nchi ya Mali iliyopo magharibi mwa Afrika.

Kiwanda cha kutengenezea samani cha Madani Doumbias ni moja kati ya viwanda vikubwa na cha zamani sana mjini Bamako, mji mkuu wa Mali. Zaidi ya watu 20 walioajiriwa wanafanyakazi katika kiwanda hiki. Wanane kati ya wafanyakazi wote ni watoto, wenye umri kati ya miaka sita na kumi. Abdoulaye ana umri wa miaka 16. Tangu miaka minane iliyopita amekuwa akifanyakazi katika kiwanda hiki, na anakwenda shule iliyo karibu na hapo.

Mimi bado nasoma. kila siku saa kumi na moja asubuhi huamka. Naoga, nakunywa chai na kwenda shule. Baada ya masomo nafanyakazi hapa kiwandani. Kwa hiyo inapofika saa 11 narudi nyumbani, naoga na kuangalia kidogo televisheni. Nakwenda kulala, bila ya kurudia mafunzo niliyopata shuleni.

Maisha kama hayo mbali ya Abdoulaye yanaendeshwa na watoto wengi nchini Mali. Kinadharia ni marufuku mtoto hadi miaka 14 kufanyishwa kazi, hususan katika maeneo yenye hatari hata baada ya kutimiza miaka hiyo hawaruhusiwi kufanya kazi. Mali imeidhinisha mikataba yote ya kimataifa dhidi ya kuwafanyisha kazi watoto.

Pamoja na hayo kuna watoto wanaofanyishwa kazi katika miji mbali mbali pamoja na vijijini kila siku.

Watoto wawili kati ya watano nchini Mali wanafanyakazi mara kwa mara, unasema uchunguzi uliofanywa na shirika la kimataifa la kazi.

Abdoulaye anaendelea vizuri katika kazi kiwandani hapo. Hapa hatumiwi kinyume na utaratibu na pia hapigwi. Madani Doumbia ni meneja wa kiwanda hicho.

Hatuwapi watoto kazi ngumu. Watoto hawapaswi kufanyakazi na mashine nzito, kwasababu wanaweza kuumia. Baadhi wanataka kufanyakazi haraka, lakini tunawazuwia , kwanza ni lazima waangalie tu na kujifunza, kwa hiyo hakuna kinachoweza kuwatokea.

Wafanyakazi wa kuajiriwa katika kiwanda hicho cha samani wanawaleta watoto wao pia kazini, kwa hiari yao. Wanataka watoto wao mapema iwezekanavyo wazowee kazi. Wataalamu kama Moulaye Hassan Tall, kiongozi wa mpango wa taifa wa kuzuwia watoto kufanyishwa kazi, analiangalia suala hilo tofauti.

Watoto hapa wanafanyakazi na vifaa hatari kama nyundo, misumeno na misumari. Lakini hawana viatu, vifaa vya kuzuwakinga mikononi ama miwani ya kinga, kwa mfano wanapowaangalia baba zao wakifanyakazi za kuunga vyuma. Hali hiyo inahatarisha moja kwa moja ama kwa njia nyingine afya ya mtoto ama usalama wake.

Kwa wazazi kuwaruhusu watoto wao kufanyakazi, kunafanya udhibiti wa kazi dhidi ya watoto kuwa mgumu nchini Mali. Ni vipi mtu anaweza kuishawishi familia masikini kuachana na tabia hii, swali hili halina jibu hata kwa mpango wa taifa wa kupambana dhidi ya kufanyishwa kazi watoto. Hata si sahihi kwa mtoto kufanyishwa kazi hata kama amekuwa mkubwa vya kutosha. Wazazi wengi hawafahamu, kwanini watoto wakifika miaka 14 wanataka kufanyakazi.

Tunaishi katika nchi masikini sana, na hii inafanya kuwa vigumu, wazazi kusema, kwamba mtoto wake hawezi tena kufanyakazi. Tunahitaji taarifa za kufanyia kampeni, kuweza kuelezea, ili wazazi wafahamu, kwamba mtoto kuanzia miaka 12 ama 14 anatakiwa kwenda shule.

Anasema Moulaye Hassan Tall. Kwa Abdoulaye changamoto hizo mbili zina mwisho. Anakwenda katika shule ya ufundi mjini mkuu wa Mali, Bamako. Hivi karibuni akimaliza shule kama anaweza kuajiriwa kama mfanyakazi wa ujenzi wa majumba. Kwa hivi sasa anafikiria, kuanzisha kampuni yake binafsi. Kufanyishwa kazi watoto kwake yeye si jambo lenye matatizo.

Mwandishi Kone, Mahamadou/ZR/ Sekione Kitojo

Mhariri Mohammed Abdul Rahman.