1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya urais Afghanistan kwazua wasiwasi

Jane Nyingi/ AFPE..Picha AFP11 Septemba 2009

Marekani imeonya kuwa kuendelea kuchelewa kutatua mgogoro unaozunguka matokeo ya uchaguzi uliofanyika nchini Afghanistan huenda ukaifanya nchi hiyo kutumbukia mikononi mwa Wataliban na kundi la kigaidi la Al-qaeda.

https://p.dw.com/p/JdGb
Mfanyikazi wa tume ya uchaguzi nchini Afghanistan akiwa katika kituo cha kupigia kura.Picha: AP

Marekani imeonya kuwa kuendelea kuchelewa kutatua mgogoro unaokumba matokeo ya uchaguzi uliofanyika nchini Afghanistan huenda ukaifanya nchi hiyo kutumbukia mikononi mwa Wataliban na kundi la kigaidi la Al-qaeda. Waafghanistan walipiga kura mwezi uliopita kumchagua rais kwa mara ya pili na miaka minane baada ya Marekani kuivamia Afghanistan na kuuondoa madarakani utawala wa Wataliban kufuatia shambulizi ya September 11 mwaka 2001 nchini Marekani lilodaiwa kutekelezwa na kundi la Al-Qaeda.

Uchaguzi huo mkuu uliofanyika tarehe 20 mwezi uliopita wa Agosti umekumbwa na madai ya wizi wa kura, undaganyifu na idadi ndogo ya wapiga kura iliyojitokeza kulaumiwa kutokana na tishio lilotolewa na wapiganaji wa kundi la Wataliban. Richard Holbrooke, mshauri wa rais Barack Obama juu ya masuala ya Afghanistan na Pakistan, ameliambia shirika la habari la BBC kuwa watakaonufaika kutokana na kuchelewa kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo ni Watalibana na mtandao wa Al-qaeda.

Marekani imesema itachukua miezi kadhaa kujua matokeo ya uchaguzi huo wa Agosti 20 ambao ni wa pili kumchagua rais. Rais Hamid Karzai anatarajiwa kupata ushindi wa zaidi ya asilimia 54 ya kura zilizohesabiwa kufikia sasa.

Mpizani wake wa karibu , waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Afghanistana, Abdullah Abdullah, anafuata kwa kupata chini ya asilimia 30 ya kura, huku akidai kulikuwa na njama za udanganyifu zilizopangwa na serikali kuhakikisha Hamid Karzai anarejea tena madarakani kwa muhula wa pili wa miaka mitano.

Hata hivyo, Holbrooke amesema shughuli hiyo lazima iungwe mkono, lakini kufutiliwa mbali kwa matokeo hayo ni jambo lisilowezekana. Matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kutangazwa siku ya jumamosi, huku jamii ya kimataifa ikiwaomba maafisa kuhakikisha haki inazingatiwa ili mshindi kamili atangazwe ili kuimaliza hali mbaya ya kisiasa iliko hivi sasa nchini humo.

Mengi ya masaduku ya kupigia kura zinazotiliwa shaka ni kutoka ngome ya Karzai, 51 kati yao ni kutoka vituo vya kupigia kura kusini kwa Kandahar, mkoa anakotokea Karzai. Nae waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza, David Miliband, ameelezea imani yake kwa tume ya uchaguzi nchini Afghanisatn na kusema ni makosa kutoa madai bila taarifa za ushuhuda.

Amesema tume hiyo ya uchaguzi imechukua muda mrefu kukamilisha kibarua cha kuhesabu kura, jambo ambalo halieleweki na Waingereza, kwani katika mataifa yanayoendelea matokeo ya uchaguzi hutangazwa baada ya masaa ya kumalizika upigaji kura.

Wakati huo huo, Majeshi ya Pakistan yamemkamata msemaji wa kundi la Wataliban na makamanda wengine wanne wa kundi hilo katika bonde la Swat. Majeshi hayo yalianzisha mashambulio yao katika bonde hilo la Swat mwezi Mei baada ya kundi la Taliban kuchukua usimamizi wake, kufutia miaka miwili ya mashambulio. Eneo hilo liko karibu na mpaka wa Pakistan na Afghanistan,ambapo makundi ya kigaidi ya Al-qaeda na Taliban yanaendesha harakati zao kwa muda mrefu sasa.

Mwandishi:Jane Nyingi/ APE

Mhariri:Othman Miraji