1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuanzia Juni 7 chanjo kwa wote Ujerumani

18 Mei 2021

Waziri wa Afya wa Ujerumani, Jens Spahn amesema kuanzia Juni 7, serikali itafungua wigo wa kutoa chanjo kwa kila mmoja nchini humo,

https://p.dw.com/p/3tWnp
Coronavirus - Impfung in Berlin
Picha: Wolfgang Kumm/dpa/picture alliance

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Berlin, waziri huyo amesema hatua hiyo haimaanishi kwamba kila moja ataweza kupata chanjo mara moja lakini atapata ahadi ya kutimiziwa takwa lake. Amesema kampeni ya chanjo imekuwa ikiendelea kwa kasi katika wiki za hivi karibuni na matarajio yake ni kwamba hadi mwishoni mwa Mei, takribani asilimia 40 ya Wajerumani watakuwa wamepata japo dozi ya mwanzo ya chanjo.

Asilimia 70 ya watu wanaopindukia miaka 60 wamechanjwa Ujerumani.

Coronavirus PK Gesundheitsminister Spahn
Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens SpahnPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Asilimia 70 ya watu wa umri uliopindukia miaka 60 wamepata dozi ya kwanza, na wengine wengi wamekamilika dozi zote mbili. Kwa ujumla dozi milioni 40 za virusi vya corona zimetolewa miongoni mwa idadi jumla ya watu milioni 83 wa Ujumerumani.

Baada ya miezi kadhaa ya marufuku kali ya kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona viwango vya maambukizi pia vinatajwa kuanza kupungua na kwa namna ya taratibu sana baadhi ya majimbo yameanza kufungua shughuli mbalimbali za kawaida.

Wakati huohuo, chombo chenye dhamana ya udhibiti wa dawa barani Ulaya-EMA kimesema ni salama kwa chanjo ya Pfizer kuhifadhiwa katika jokofu hadi siku 30, katika kile kinachoitwa uamuzi utakatoa urahisi wa usambazaji wa chanjo hiyo katika maeneo tofauti ya mataifa ya Ulaya.

Mapema mwezi huu, Umoja wa Ulaya umekubali kuingia katika makubaliano makubwa na makampuni ya utengenezaji wa chanjo hiyo ya Pfizer na BioNtech ya ununuzi wa dozi bilioni 1.8 ya hadi 2023.

Marekani imeahidi kutoa dozi milioni 20 kwa mataifa yenye uhitaji.

Wasafari kutoa katika maeneo tofauti ya Ulaya wameanza kuwasili nchini Italia baada ya taifa hilo kuondoa masharti ya kuwaweka karantini wasafiri kutoka katika mataifa ya Umoja wa Ulaya, Israel na Uingereza.  Na shirika la afya duniani WHO, limesema Rais Joe Biden wa Marekani atatoa nje ya mipaka ya taifa lake takribani dozi milioni 20 ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao, ikiwa ni mara ya kwanza kwa taifa hilo kutoa hifadhi ya chanjo yake kwa mataifa ya nje kwa zingatio la mpango wa msaada wa chanjo kwa mataifa yenye uhitaji unaoratibiwa na WHO wa ujulikanoa kama Covax.

Nchini Taiwan serikali ya taifa hilo imesema ipo katika matarajio ya kutoa chanjo ambayo itazalishwa katika taifa hilo kwa watu wake ifiakpo mwezi Julai.