1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuala Lumpa:Mkutano wa nchi za Asia.

28 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG3M

Katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpa kunakoendelea mkutano wa usalama wa nchi za Asia, uliohudhuriwa na nchi 25 zenye polisi wa dunia katika maeneo kadhaa ulimwenguni, kumegubikwa na mada kuu kuhusu vita vya mashariki ya kati na mpango wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini na Iran.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleezza Rice amehudhuria kwa mara ya kwanza mkutano huo wa Asia, utakaozungumzia mgogoro wa Mashariki ya kati na mpango wa Nuklia wa Pyongyang, licha ya Korea ya Kaskazini yenyewe kutoshiriki katika mazungumzo hayo.

Aidha Korea ya Kaskazini imetishia kuondoka katika mkutano huo ikiwa jaribio lake la misiles la hivi karibuni litalaumiwa na wajumbe wa mkutano huo.