Kuachiwa mateka nchini Colombia kwacheleweshwa tena
30 Desemba 2007Shirika la msalamba mwekundu nchini Colombia limesema kuachiwa huru mateka watatu akiwemo mtoto wa umri wa miaka mitatu, ambao wamekuwa wakizuiliwa na waasi wa kimaksi katika msitu nchini Colombia, kumecheleweshwa kwa siku ya pili huku jamaa wa familia zao na wajumbe wa kimataifa wakisubiri kwa hamu kubwa kuachiliwa kwao.
Helikopta mbili zilizotumwa na rais wa Venezuela, Hugo Chavez, ambaye ameongoza juhudi za kuwaokoa mateka hao kupitia ushirikiano wa shirika la msalaba mwekundu, zimekuwa zikisuburi katika mji wa Villavicencio nchini Colombia tangu juzi Ijumaa.
Huku matumaini ya kuachiwa huru mateka hao yakipungua rais Hugo Chavez amesema baada ya kushauriana na maafisa wanaoshughulikia kuachiwa huru mateka hao kwamba mateka hao huenda wakaachiwa hivi leo au kesho.