SiasaKorea Kusini
Korea Kusini yathibitisha kurejesha mahusiano na Japan
21 Machi 2023Matangazo
Hayo ni wakati nchi hizo mbili zikiimarisha mahusiano yao kufuatia kuongezeka vitisho kutoka Korea Kaskazini.
Hatua hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Korea Kusini imefuatia mkutano wa kilele kati ya viongozi wa nchi hizo, rais Yoon Suuk Yeol wa Korea Kusini na waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida mjini Tokyo wiki iliyopita.
Soma pia: Japan na Korea Kusini zatangaza hatua za kurejesha uhusiano
Kupitia mazungumzo hayo yaliyofanyika baada ya miaka 12, nchi hizo zilikubaliana kurudisha mahusiano mazuri yaliyoharibiwa na mivutano ya kihistoria iliyotokana na utawala wa miaka 35 wa kikoloni wa Japan katika rasi ya Korea.