Korea kusini nayo yachukua hatua
19 Oktoba 2008Matangazo
Seoul:
Korea kusini imetangaza mpango mkubwa wa kuipa msukumo sekta ya mabenki nchini humo. Serikali imesema itachuku dhamana ya madeni ya fedha za kigeni ya mabenki nchini humo ya hadi dola bilioni 100. Pia imesema kwamba itatoa dola nyengine bilioni 30 kwa mabenki yanayokumbwa na msukosuko, pamoja na makampuni mengine.Sarafu ya Korea kusini imekumbwa na wasi wasi wa wawekezaji, ikihofiwa kwamba huenda uchumi wake ukashindwa kupata dola inazohitaji kulipia madeni yake ya kigeni, pamoja na kwamba nchi hiyo ni ya sita miongoni mwa zile zenye akiba kubwa ya fedha za kigeni duniani.Korea kusini imejiunga na nchi kadhaa na kuahidi kutoa msaada mkubwa kuyanusuru mabenki, kutokana na msuko suko wa fedha duniani.