1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea kaskazini yatengeneza bomu la Haidrogeni

Sekione Kitojo
3 Septemba 2017

Korea kaskazini imesema leo Jumapili(03.09.2017)imetengeneza bomu la haidrojeni lenye "uwezo mkubwa wa maangamizi" wakati rais Trump na waziri mkuu wa Japan Abe wamezungumza kwa simu juu ya ongezek la mzozo  wa nyuklia.

https://p.dw.com/p/2jH3L
Nordkorea Kim Jong Un bei Besuch einer Fabrik für Nuklearwaffen
Picha: Reuters/KCNA

Ripoti hiyo iliyotolewa  na shirika  rasmi la  bahari la Korea  kaskazini KCNA inakuja wakati  kuna  hali ya juu  ya  wasi  wasi  katika eneo hilo kufuatia majaribio mawili ya  makombora yanayoweza  kuvuka bara moja  hadi  jingine mwezi Julai ambayo yana uwezo  wa  kuruka kiasi  ya  kilometa 10,000 , na  kuyaweka  maeneo  mengi  ya Marekani  kuweza  kufikika.

Chini  ya  kiongozi  wa  kizazi  cha  tatu Kim Jong Un , Korea kaskazini  imekuwa  ikiwania  kutafuta  silaha  za  kinyuklia  ndogo na  nyepesi kuweza  kuwekwa  katika  kombora la  masafa  marefu, bila  kuathiri uwezo  wake  wa  kuruka  na  kulifanya   kuwa  na uwezo  wa  kuhimili  kuingia  katika  anga la  dunia.

Nordkorea Kim Jong Un bei Besuch einer Fabrik für Nuklearwaffen
Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un akitoa maelezo kuhusu silaha za kinyukliaPicha: Reuters/KCNA

Korea  kaskazini , ambayo  inafanya  mipango  yake  ya  makombora na  nyuklia  kwa  kukaidi  maazimio  na  vikwazo  vya  baraza  la Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa , "hivi  karibuni  ilifanikiwa" kuitengeneza  bomu  la  hali  ya  juu  kabisa  la  haidrojeni  ambalo linaweza  kuwekwa  katika  kombora  la  masafa  marefu  la  ICBM, limesema  shirika  hilo  la  habari  la  KCNA.

Bomu  hilo  la  haidrojeni , uwezo  wake  wa  kuripuka  ambao unaweza  kurekebishwa  kutoka  mamia  ya  kilotani  na  kuwa maelfu  ya  kilotani, ni  bomu  la  nyuklia  lenye  uwezo  wa  aina mbali  mbali  na  uwezo  mkubwa  wa  maangamizi  ambalo  linaweza kuripuriwa  hata  katika  kima  kirefu  kwa  kutumia  vifaa  vyenye nguvu  kubwa  ya  shambulizi  vya  EMP , (electromagnetic pulse) kwa  mujibu  wa  lengo  lake  la  kimkakati, shirika  la  habari  la KCNA  limesema.

Nordkorea Raketenstart
Kombora la Korea kaskazini likivurumushwa Picha: Reuters/KCNA

Korea kaskazini haijatoa ushahidi

Hata  hivyo  Korea  kaskazini haijatoa ushahidi  wa  madai  yake  ya hivi  karibuni, na  Kim Dong-yub , mtaalamu  wa  kijeshi  katika  chuo kikuu  cha  Kyungnam wa mitaala  ya  mashariki  ya  mbali  mjini Seoul, ameonesha  shaka.

"Akizungumzia  kuhusu mamia  kwa  maelfu ya  kilotani , haionekani kuzungumzia  kuhusu  bomu  hilo  la  haidrojeni. Inawezekani  ni chombo  kilichoboreshwa, amesema Kim, alizungumzia  kuhusu bomu  la  atomic  ambalo  linatumia  gesi  ya  haidrojeni kuimarisha mripuko.

Bomu  la  haidrojeni  linaweza  uwezo  wa  kuripuka  wa maelfu  ya kilotani , ikiwa  na  nguvu  zaidi  kuliko kilotani 10 hadi 15  ambazo jaribio  la  mwisho  la  kinyuklia  la  Korea kaskazini  ilifanya  mwezi Septemba  ambalo  ilikadiriwa  kutengeneza, sawa  na  bomu lililodondoshwa  mjini  Hiroshima , Japan  mwaka 1945  na Marekani.

Nordkorea Militärparade Symbolbild
Makombora ya Korea kaskaziniPicha: Getty Images/AFP/E. Jones

Kim Jong Un, ambaye  ametembelea  taasisi  ya  nchi  hiyo  ya kinyuklia, "aliangalia  bomu  la  haidrojeni litakalowekwa  katika kombora  linalokwenda  masafa  marefu na "kuweka mkakati  wa kukamilishwa  kwa  utafiti  kuhusu  nyuklia," shirika  la  habari  la KCNA  limesema.

Picha  zilizotolewa  na  shirika  hilo  la  habari  zinamuonesha  Kim akikagua  silaha  yenye  rangu  ya  fedha   katika  ziara  hiyo akifuatana  na  wanasayansi  wa  nyuklia , wakiwa  na  mchoro  wa kombora  la  Hwasong-14 likionekana  ukutani.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre

Mhariri: Sudi Mnette