Korea Kaskazini yarejesha shughuli za kijeshi mpaka na Seoul
27 Novemba 2023Matangazo
Wiki iliyopita Korea Kusini ilisema itayasitisha kwa muda makubaliano na jirani yake Kaskazini na kuanza tena operesheni ya kufuatilia matukio kwenye eneo la mpaka kufuatia kitendo hicho cha Korea Kaskazini.
Korea Kusini imeitaja hatua yake hiyo kama mipango ya kujilinda kufuatia hatua iliyochukuliwa na jirani yake.
Soma pia: Marekani na Korea Kusini zarekebisha makubaliano ya kuikabili Korea Kaskazini
Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini pia imesambaza kwenye vyombo vya habari picha inazosema zinaonesha shughuli za kijeshi katika eneo la mpaka upande wa Kaskazini.
Rais Yoon Suk Yeol ametoa amri, jeshi la nchi hiyo lifuatilia kwa karibu kinachoendelea na kujiweka katika hali ya tahadhari.