SiasaKorea Kusini
Korea Kaskazini yaionya Korea Kusini juu ya luteka za jeshi
17 Februari 2023Matangazo
Luteka hizo zitafanyika mjini Washington, ambapo washirika hao, Marekani na Korea Kusini watajadili jinsi ya kujibu ikiwa Korea Kaskazini itatumia silaha za nyuklia. Kwa muda mrefu Korea Kaskazini imekuwa ikiyapinga mazoezi ya pamoja baina ya nchi hizo, ikisema ni matayarisho ya uvamizi.
Tangazo la serikali ya mjini Pyongyang limesema ikiwa Marekani na Korea Kusini zitaendelea na mipango hiyo, zitajibiwa vikali tena kwa muda mrefu.
Chini ya uongozi wa rais mwenye msimamo mkali, Yoon Suk Yeol, Korea Kusini imeimarisha mazoezi ya kijeshi ya pamoja na Marekani, ambayo yalikuwa yamepungua wakati wa janga la Uviko.