Korea Kaskazini yakosoa luteka za kijeshi za Marekani
22 Agosti 2023Mazoezi hayo yaliyofunguliwa jana Jumatatu yanajumuisha onesho la kukabiliana na kitisho cha nyuklia cha Korea Kaskazini .
Katika maoni yaliyochapishwa na shirika la habari la Korea Kaskazini, serikali mjini Pyongyang imelaani luteka hiyo ya kijeshi ya msimu wa kiangazi pamoja na na mkutano uliofanyika hivi karibuni kati ya Marekani, Korea Kusini na Japan nchini Marekani.
Korea Kaskazini imesema makubaliano yaliyofikiwa baina ya mataifa hayo matatu washirika yanatishia kuzusha vikali vya nyuklia kwenye rasi ya Korea.
Kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye makaazi ya mapumziko ya rais wa Marekani huko Camp David, viongozi wa nchi hizo tatu waliafikiana kuimarisha ushirikiano wa kiusalama na kiuchumi kama sehemu ya mpango wa kushuhuglikia kitisho cha Korea Kaskazini na kutanuka kwa nguvu za China.