Korea Kaskazini yaadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwake
9 Septemba 2023Korea Kaskazini leo imefanya kumbukumbu ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwake kwa gwaride kubwa la kijeshi, lililoshuhudiwa na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un.
Kim ametumia maadhimisho ya leo kufanya mazungumzo na ujumbe wa wanadiplomasia waliofika na kuapa kuimarisha ushirikiano na nchi za China na Urusi.Pyongyang yafanya mazoezi ya mbinu za shambulizi la nyuklia
Vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kwamba viongozi wa China na Urusi wamemtumia ujumbe wa barua Kim wa kuimarisha ushirikiano wa pande mbili haswa katika masuala ya kiusalama na utulivu katika rasi ya Korea na Kaskazini mashariki mwa Asia.
Kim anatarajiwa kuitembelea Urusi baadae mwezi huu atakapokutana na Rais Vladimir Putin kujadili juu ya usambazaji wa silaha kwa Moscow ili kusaidia katika vita vyake huko Ukraine.