Wakati uandikishaji wa wapiga kura ukiendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, chama cha PPRD cha rais wa zamani Joseph Kabila na FCC, ambao ni muungano wa vyama vinavyomuunga mkono, vimeisusia operesheni hiyo iliyoanza Desemba 24 katika mikoa kumi ya nchi hiyo. Mwandishi wetu kutoka Kinshasa Jean Noël Ba-Mweze alituandalia ripoti hii kwa urefu.