Kongamano juu ya uwekezaji Afrika Mashariki
29 Julai 2009Matangazo
Kongamano hilo la siku tatu lililofunguliwa na Marais wa Jumuiya hiyo linahudhuriwa na zaidi ya wajumbe elfu moja wakiwemo wawekezaji na wanabiashara kutoka Afrika, Ulaya na Marekani.
Mkutano huo ambao ni wa pili kufanyika tangu jumuiya hiyo ifufuliwe ni kuwahamasisha wawekezaji juu ya nafasi zilizopo
za uwekezaji katika eneo zima la Afrika Mashariki na kutafuta mbinu za kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi inayoshuhudiwa kote Duniani.
Mwandishi wetu kutoka Nairobi Alfred Kiti ametuandalia taarifa ifuatayo.
Mtayarishaji:Alfred Kiti
Mpitiaji:Othman Miraji