1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombora la Korea Kaskazini lakosa Mafanikio

13 Aprili 2012

Korea ya Kaskazini imekiri zoezi lake la kulifyatuwa angani kombora la masafa marefu limeshindwa katika kile kinachoonekana kuaibika hadharani. Shughuli hiyo iliibua shutuma kali kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

https://p.dw.com/p/14dSV
09/04/2012 ; PYONGYANG, North Korea - Photo taken April 8, 2012, shows the Unha-3 rocket at its launch pad at the Sohae Satellite Station in Tongchang-ri, North Pyongan Province in the northwest of North Korea. In a rare move, Pyongyang allowed foreign media organizations, including Kyodo News, a firsthand look at preparations under way for what it says is the launch of a long-range rocket for putting a satellite into space, which is viewed by the United States and its allies as a disguised test of ballistic missile technology. Photo: MaxPPP/Kyodo pixel
Nordkoreanische Rakete auf dem Startgelände von Tongchang-riPicha: picture-alliance/dpa

Kukiri huko ni nadra kufanywa na taifa hilo kukiwa ni pigo kwa kiongozi kijana Kim Jong Un, anayeshutumiwa na jumuiya kimataifa kwa kufanya jaribio hilo. Korea Kaskazini imesema kumekuwepo na kutiwa chumvi kwa kushindwa kwao ambapo kulikwenda sambamba na kusherehekea miaka 100 tangu kuzaliwa kwa kiongozi mwanzilishi wa taifa hilo Rais Kim II Sung, kwa sasa taifa hili linaongozwa na mjukuu wake.

Wakati huu, ulimwengu ukitarajia kufanyika kwa jaribio lingine la tatu kwani Korea Kaskazini inataka kuionyesha dunia kuwa ina uwezo mkubwa wa kijeshi. Hilo ni pigo kwa kiongozi kijana Kim Jong Un, anayeshutumiwa na jumuiya kimataifa kwa kufanya jaribio hilo.

Kombora hilo la masafa marefu liliruka umbali usiziodi kilomita 100 na kuripuka baharini jirani na rasi ya Korea na China likiwa limeshindwa kufikia mafanikio ya kombora la mwaka 2009 ambalo lilisafiri umbali wa kilometa 3800.

Maandamano yalifanywa kupinga mpango huo wa kombora la Korea Kaskazini mjini Seoul, Korea Kusini
Maandamano yalifanywa kupinga mpango huo wa kombora la Korea Kaskazini mjini Seoul, Korea KusiniPicha: Reuters

Marekani na Japan kwa pamoja zimedai kuwa kutofanikiwa kwa Korea ya Kaskazini ni jambo linaloibua maswali mengi juu ya taifa hilo linalodhaniwa kuwa na uwezo mkubwa kijeshi huku likishindwa kuwalisha wananchi wake na muda wote kutegemea misaada kutoka nje. Ujerumani imetoa tamko juu ya kitendo hicho. Akiwa Marekani Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle alisema kushindwa jaribio hilo ni pigo kwa Korea ya kaskazini.

Akaongeza kuwa "Tunalaani kuzinduliwa kwa jaribio hilo, kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria la kimataifa na tunadhani kwa sasa ni vizuri Baraza la Usalama la umoja wa mataifa kutoa jawabu ya jinsi Korea ilivyokiuka sheria hizo."

Kutokana na ukaidi wake na kukiuka sheria za kimataifa kumekuweko na ushauri juu ya taifa hilo kuongezewa vikwazo vya kimataifa lakini kikwazo kikubwa ni China ambayo kwa hakika inaonekana wazi kutokubaliana na ushauri huo, japokuwa yenyewe imeshindwa kuishawishi Korea kaskazini. Kwa upande wake kiongozi wa sasa kijana wa taifa hili Kim Jong Un, ameweka bayana kuwa anatumai mwaka 2012 kuwa mwaka ambao utaonyesha ulimwengu kuwa Korea ya Kaskazini ni taifa imara na litakaofikia mafanikio makubwa dunia.

Mwandishi:Adeladius Makwega

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman