1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Dunia la Kandanda laenda Ujerumani

Maja Dreyer1 Oktoba 2007

Leo Wajerumani kweli wanafurahi na kuwasubiri mabingwa wao wachezaji wanawake wa kandana ambao walishinda kwenye kombe la dunia jana huko China. Wahariri wa magazeti pia wanawashangilia wachezaji hao.

https://p.dw.com/p/CHRj
Wachezaji wanasheherekea ushindi wao
Wachezaji wanasheherekea ushindi waoPicha: AP

La kwanza ni gazeti la “Volksstimme” la mjini Magdeburg. Limeandika:

“Timu hiyo imetetea ubingwa wake wa dunia. Hiyo haijawahi kutokea katika kandana la wanawake. Juu ya hayo, kwa mara ya kwanza katika historia, timu imeshinda bila ya kufungwa hata goli moja. Basi, kombe hilo la mchezo wa mpira litalipigia debe kandanda la wanawake nchini humu. Pia linaongeza matumaini ya kupata kombe hilo kwenye mashindano ya mwaka 2011 yatakayofanyika hapa Ujerumani.”

Karibu mashabiki Millioni 12 wa soka hapa nchini walifuatilia fainali hiyo kupitia televeshi zao hapo jana. Mhariri wa “Nürnberger Zeitung” ambaye bila shaka alikuwa miongoni wa watazamaji anazichambua hivi takwimu hizo:

“Pamoja na wengine hasa ni fanikio ya kocha wa timu ya wanawake, Bi Sylvia Neid, kwamba idadi ya mashabiki wa kandanda la wanawake imeongezeka sana. Bado wanawake hawana mashabiki wengi kama huko Marekani au China. Lakini mechi hiyo ya fainali ambayo ilichezwa vizuri kweli kweli imeipatia ungaji mkono mkubwa timu ya taifa ya wanawake. Na kocha Bi Neid atafurahshwa na haya.”

Licha ya mafanikio kwenye mashindano ya kombe la dunia, gazeti la “Tageszeitung” la mjini Berlin linalaumu kuwa mchezo wa mpira wa wanawake bado haupewi umuhimu wa kutosha. Limeandika:

“Bado wachezaji hao wanawake hawawezi kuishi juu ya mapato yao kwenye michezo. Wengi wao wana ajira nyingine na ni wachache tu ambao kama wachezaji wa timu ya taifa walipata mikataba ya kutengeza matangazo. Basi ni juu ya klabu za Bundesliga kujenga mbinu za kitaalumu, kujipatia wafadhili wa kuijenga kabisa ligi hiyo. Hadi leo mechi za wanawake hazionekani ila tu zile za mashindano ya kombe la dunia kila baada ya miaka minne. Hali hii ibadilishwe!”

Na kwa suala la pili linalozingatiwa kwenye kurasa za wahariri hii leo tuelekee Afghanistan ambapo rais Hamid Karzai aliwaalika Wataliban kwenye meza ya mazungumzo. Maoni juu ya hatua hiyo yanatofautiana. Yafuatayo ni ya mhariri wa “Frankfurter Allgemeine Zeitung”:

“Inaonekana kama rais Karzai amevunjwa moyo kabisa juu ya mauaji mengine yaliyotokea Kabul kwamba si tu alitoa mwito kwa viongozi wa Taliban kushiriki kwenye mazungumzo bali pia aliahidi kuwapa nafasi kwenye serikali. Lakini wakati Wataliban wanatumia mkakati wa kigaidi, ni jambo lisilofahamika kuona kuwa Karzai yuko tayari kupatana na kundi hilo linaloiharibu nchi.”

Msimamo mwingine juu ya hatua ya rais Karzai wa Afghanistan tunaosoma katika gazeti la “Die Welt”:

“Kwa muda mrefu kupatana na Wataliban kulikuwa kitu kisichozungumzwa. Sasa lakini imefahamika kwamba katika jamii ya Afghanistan kuna baadi ya makabila ambayo yako tayari kutafuta mwafaka ili kujipatia mamlaka ya halali na kufanya biashara bila ya kusumbuliwa. Huenda Karzai atafanikiwa kuwagawa Wataliban na wale wanaowaunga mkono.”