Kombe la Dunia 2018: Timu 32 zinazoshiriki
Jumla ya mataifa 32 yatawakilishwa katika Kombe la Dunia la FIFA nchini Urusi. DW inaagalia timu zote zitakazokuwa katika mashindano hayo ya 2018
Urusi
Urusi ilifuzu katika dimba hilo moja kwa moja kama wenyeji na itakuwa mara yao ya 11 kushiriki katika Kombe la Dunia. Walishindwa kufuzu kutoka Kundi lao wakati wa Kombe la Shirikisho mwaka 2017, baada ya kushindwa na Ureno na Mexico, ijapokuwa waliwazaba New Zealand
Brazil
Brazil hawajawahi kushindwa kufuzu kazika Kombe la Dunia kwa mara 21 na walimaliza wa kwanza katika michuano ya kufuzu ya Amerika Kusini. Pia wameshinda Kombe la Dunia mara tano – kuliko taifa jingine lolote – na mashambulizi yao yataongizwa na nyota wa Paris Saint-Germain Neymar, wakati wakilenga kubeba taji lao la sita
Uhispania
Washindi wa Kombe la Dunia 2010 na Mabingwa wa Ulaya 2008 na 2012 walijikatia tikiti ya kwenda Urusi wakisalia na mechi moja ya kucheza. Uhispania walifanikiwa kufunga mabao mengi katika safari ya kufuzu na wanapigiwa upatu na wengi kutamba Urusi
Ufaransa
Ufaransa walicheza fainali ya Euro 2016 na hawana upungufu wowote wa wachezaji nyota. Walifuzu kwa kuongoza Kundi A ambalo Uholanzi ilishindwa kufuzu. Joachim Löw anawaona Ufaransa kuwa wapinzani wa wazi wakati Ujerumani ikilenga kutetea taji lao.
Ureno
Licha ya safari ngumu ya kufuzu, Cristiano Ronaldo atakwenda Urusi kucheza dimba la Kombe la Dunia. Ureno ilipata tikiti ya moja kwa moja na sio Uswisi baada ya kuwazaba wenzao hao wa Kundi B. Akiwa na umri wa miaka 32, inaaminika kuwa Urusi huenda ikawa Kombe la Dunia la mwisho la CR7, baada ya kushinda Euro 2016 na nchi yake.
Iceland
Iceland walijipatia nafasi ya kucheza mashindano ya kimataifa kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuwaondoa England katika Euro 2016. Kwa hiyo jiandane kuwashangilia nchini Urusi. Gylfi Sigurdsson, ndiye mchezaji nyota wa Iceland, lakini ana kikosi imara kinachoshirikiana naye. Iceland ilishinda Kundi I, mbele ya Croatia, Ukraine na Uturuki
Serbia
Serbia iliongoza Kundi D ikiwa na pointi 21, kwa kuwazaba Georgia katika mechi ya mwisho ya makundi na kujikatia tikiti ya Kombe la Dunia. Walishiriki mara ya mwisho 2010. Hii iliwafanya kusherehekea kwa hisia nyingi huku kungo nyota wa Manchester United Nemanja Matic akitiririkwa na machozi
Nigeria
The Super Eagles walikuwa timu ya kwanza ya Afrika kufuzu baada ya kombora la Alex Iwobi dhidi ya Zamba kuhakikisha kuwa wanaongoza Kundi B. Mchezaji huyo wa Arsenal ni mmoja wa wachezaji sita wa Premier League katika timu ya sasa lakini, licha ya kushinda mwaka wa 2013, Nigeria wameshindwa kufuzu katika mashindano mawili yaliyopita ya Kombe la Afrika. Urusi itakuwa Kombe lao la saba kushiriki
Japan
Japan lifuzu kucheza Kombe la Dunia kwa kuongoza Kundi B barani Asia mbele ya Saudi Arabia na Australia. Itakuwa mara yao ya sita kushiriki katika Kombe la Dunia ambapo hawajawahi kupita hatua ya 16 za mwisho.
Ujerumani
Mabingwa hao wa sasa walifuzu kwa urahisi katika Kombe la Dunia la Urusi. Ushindi katika Kombe la Shirikisho na mashindano ya Euro kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 ulidhihirisha umahiri wa timu ya Ujerumani na wataingia Urusi kama mojawapo ya timu zinazotarajiwa kutamba
Costa Rica
Bao la dakika za mwisho la kichwa kutoka kwa Kendall Watson liliwapa tikiti Costa Rica kucheza kwa mara yao ya nne kati ya mashindano matano ya mwisho ya Kombe la Dunia. Taifa ya hilo la America ya Kati liliishinda Marekani na kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Mexico. Urusi itakuwa ni Kombe lao la tano kushiriki. Walifika robo fainali 2014
Mexico
Mexico wamefuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara 16, baada ya kumaliza wa kwanza katika mechi za kufuzu za CONCACAF mbele ya Costa Rica. Wamexico walitinga robo fainali 1970 na 1986. Huenda watamtegemea sana aliyekuwa mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Chicharito ambaye anachezea West Ham katika Premier League
Iran
Washindi hao wa Kundi A la bara Asia walikuwa timu ya tatukujitia tikiti ya kwenda Urusi, baada ya Brazil na wenyeji. Chini ya ukufunzi wa aliyekuwa kocha wa Real Madrid Carlos Queiroz, timu hiyo iliweka rekodi mpya ya kufuzu, baada ya kucheza mechi 12 bila kufungwa bao kabla ya kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Syria katika mechi yao ya mwisho. Hili ni Kombe lao la tano la Dunia kushiriki
England
Licha ya rekodi ya kutoshindwa katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia ambayo inarudi miaka nane iliyopita na mechi 38, kila kitu sio shwari katika kikosi cha England. Fedheha ya Euro 2016, kisha uongozi wa mechi moja wa Sam Allardyce vimewaacha wengi wakiwa bila matumaini. Lakini washindi hao wa 1966 wanacheza Kombe lao la Dunia kwa mara ya 5 mfululizo.
Saudi Arabia
Record imara ya mechi za nyumbani iliwasaidia the Saudi Arabia kupata tikiti ya kucheza Kombe la Dunia kwa mara yao ya tano. Mashabiki wa Ujerumani watakuwa na kumbukumbu za furaha dhidi ya Saudi Arabia katika Kombe la Dunia – waliwazaba mabao 8 katika mechi yao ya ufunguzi ya dimba la 2002.
Korea Kusini
Korea Kusini pia ilifuzu mapema kwa kutoka sare ya 0-0 na Uzbekistan na ni mara yao ya kumi kucheza katika tamasha hilo la kimataifa. Wenyeji wa dimba hilo la 2002 ambao walifika nusu fainali walipoteza mechi 3 kati ya 10 na kufunga mabao 11 pekee. Nyota wa Tottenham Son Heung-min atakuwa kitisho katika timu hiyo
Ubelgiji
Huku ikiwa na wachezaji wengi nyota wakiwemo Eden Hazard, Romelu Lukaku, Kevin de Bruyne na Dries Mertens, Ubelgiji walizufu wakiwa wamebaki na mechi mbili za kucheza. Baada ya kutinga robo fainali ya 2014, The Red Devils walikuwa na matokeo mabaya katika Euro 2016 walipotimuliwa mikononi mwa Wales katika hatua ya nane za mwisho
Misri
Misri ilifuzu katika Kombe la Sunia kwa mara ya kwanza tangu 1990, na nusra nafasi hiyo iiendee Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Misri walihitaji ushindi na bao la penalty katika dakika za majeruhi kutoka kwa Mo Salah lilihakikisha wanashinda 2-1 na kuzusha sherehe na shangwe uwanjani na mji mkuu Cairo
Poland
Poland ilipata tikiti yao ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 2006 baada ya kuishinda Montenegro 4-2. Mshambuliaji matata wa Bayern Munich Robert Lewandowski, aliibuka mfungaji bora wa Ulay katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia baada ya kufunga mabao 16
Argentina
“Niliiambia timu: Messi hana deni la Kombe la Dunia kwa Argentina, bali kandanda lina deni la Kombe la Dunia kwa Messi”, yalikuwa maneno ya kocha wa Argentina Jorge Sampaoli baada ya hat trick Lionel Messi dhidi ya Equardor – ya 44 katika taaluma yake – kuhakikisha Argentina inacheza Kombe la Dunia.
Panama
Panama wanacheza Kombe lao la kwanza la Dunia, baada ya kufuzu mbele ya Marekani. Baada ya kushindwa kufuzu katika dimba lililopita kwa kufungwa na Marekani mabao mawili katika dakika za nyongeza mwaka wa 2013, taifa hilo lilihakikisha mara hii linaweka mambo sawa. Waliwafunga Costa Rica bao ambalo halikuonekana kuvuka mstari wa goli katika dakika ya 87
Colombia
Nyota wa dimba lililopita la Kombe la Dunia James Rodriguez, atapata fursa nyingine kuonyesha kipaji chake katika jukwaa la kimataifa baada ya Colombia kufuzu kwa kutoka sare ya 1-1 na Peru. Rodriguez, anayechezea Bayern Munich aliiweka Colombia kifua mbele katika mechi hiyo
Uruguay
Uruguay, wenyeji wa kwanza kabisa wa Kombe la Dunia kuwahi kushinda Kombe hilo, watacheza kwa mara yao ya 13. Luiz Suarez alifunga mara mili wakati wakipata tikiti ya moja kwa moja kwa ushindi wa 4-2 dhidi ya Bolivia. Wanatuhumiwa kwa kuwa na kikosi cha wazee lakini kocha Oscar Tabarez amefaulu kuchanganya na wachezaji chipukizi, katika mashindano ya 2010 na 2014.
Tunisia
Tunisia walijihakikishia nafasi katika Kombe la Dunia nchini Urusi baada ya kumaliza wa kwanza katika Kundi A. Timu hiyo ya kocha Nabil Maaloul ilitoka sare ya 0-0 dhidi ya Libya katika mechi yao ya mwisho ya makundi na kuhakikisha kuwa wanamaliza pointi moja juu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Yatakuwa mashindano yao ya tano kushiriki
Morocco
Morocco ilifuzu katika Kombe la Dunia wakiongoza Kundi C bila kufungwa bao hata moja, na kuizaba Ivory Coast mabao mawili kwa sifuri katika mechi yao ya mwisho ya makundi. Waliondolewa katika hatua ya mchujo ya Kombe la Dunia la 1986 na free kick ya Lothar Matthäus
Uswisi
Baada ya kumaliza nyuma ya Ureno katika Kundi B, Uswisi walipewa mechi ngumu ya mchujo dhidi ya makamu bingwa wa Kundi C Ireland ya Kaskazini. Aliyekuwa beki wa kushoto wa Wolfsburg Ricardo Rodriquez alifunga bao pekee la ushindi na kuwapa Waswisi tikiti yao ya 11 ya Kombe la Dunia
Croatia
Baada ya kufuzu kutoka Kundi gumu Zaidi la I wakiwa katika nafasi ya pili nyumaya Iceland, Croatia ilipata ushindi mkubwa wa jumla ya mabao 4-1 dhidi ya Ugiriki katika mechi yao ya mchujo. Luka Modric, Nikola Kalinic, Ivan Perisic na Andrej Kramaric walifunga mabao hao ya Croatia ambao walifika nusu fainali ya 1998. Sasa wamefuzu kwa mara ya tano katika mashindano sita ya mwisho ya Kombe la Dunia
Senegal
Senegal ilifuzu katika Kombe la Dunia kwa mara yao ya pili baada ya kuongoza Kundi D kutokana na ushindo wa mfululizo dhidi ya Afrika Kusini. Simba hao wa Nyika walicheza katika Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza 2002 na wakaondolewa katika robo fainali
Sweden
Sweden iliwashangaza wengi katika mechi za mchujo za kufuzu katika dimba la Kombe la Dunia baada ya kuizaba Italia jumla ya bao 1-0. Jacob Johansson alifunga bao hilo la ushindi katika mkondo wa kwanza wakati Italia ilishindwa kufuzu katika Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1958. Kwa Sweden, itakuwa mara yao ya 12, na yao ya kwanza tangu 2006
Australia
Licha ya kushiriki katika Kombe la Dunia mara moja pekee kati ya 1930 na 2002, Australia wamefuzu sasa kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuwashinda Syria na Honduras katika mechi za mchujo za mikondo miwili. Nahodha Miles Jedinak alifunga hat trick wakati Socceroos waliwapiku Honduras jumla ya 3-1 na kujikatia tikiti ya Urusi
Denmark
Baada ya sare ya 0-0 katika mkondo wa kwanza, ilikuwa Denmark iliyopata ushindi mkubwa wa 5-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland katika mkondo wa pili wa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia. Christian Eriksen alifunga mabao matatu na kuipeleka nchi hiyo katika Kombe la Dunia kwa mara yao ya tano. Ilicheza katika mwaka wa 1986, 1998, 2002 na 2010
Peru
Winga wa zamani wa Schalke Jefferson Farfan alifunga bao wakati Peru ikitinga katika Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 35. Iliishinda New Zealand na kuwa timu ya mwisho kupata tikiti kwenda Urusi. Mara ya mwisho Peru ilifuzu katika Kombe la Dunia, Ukuta wa Berlin ulikuwa bado upo