Kombe la Challenge laanza Dar-es-salaam
7 Desemba 2007Taifa Stars jumamosi hii (Tanzania) wanafungua dimba na Harambee stars-Kenya kuania challenge cup-kombe la Afrika mashariki na kati.Nchi za kiafrika zinazoania tiketi zao za kombe lijalo la dunia 2010, zinapaswa kucheza mechi zao 4 za kwanza kila mwisho wa wiki kwa wiki 4 mfululizo-yasema FIFA.Tunawafunulia kawa za changamoto za Ligi mashuhuri barani Ulaya mwishoni mwa wiki hii::
Mjini Dar-es-salaam jumamosi hii Challenge Cup –kombe la Afrika mashariki na kati linaanza kwa kishindo: Kinyan’ganyiro hiki kitaendelea hadi dsemba 22 pale mabingwa wapya watakapotawazwa kitini.Mabingwa watetezi ni Sudan watakaocheza huko Arusha:Mbali na Kenya na Tanzania katika kundi A mjini Dar, kuna pia Burundi na Somalia.
Kundi B linalocheza pia Dar, lajumuisha Ruanda na Uganda huku kundi C huko Arusha, linawapambanisha mabingwa Sudan,jirani zao Ethiopia na chipukizi Zanzibar.
Timu za Afrika zinazoania tiketi zao kwa kombe lijalo la dunia 2010 huko Afrika kusini, kwa muujibu wa FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni,zitapaswa kuingia uwanjani wikiendi 4 tena mfululizo.
Awamu ya kwanza mechi hizo itaanza mwishoni mwa Mei na kumalizika septemba.
Wiki 4 za mwezi juni,zitatumika kwa duru 4 za kwanza za makundi mbali mbali.hii itazusha matatizo makubwa katika mipango ya kalenda za mashindani barani Afrika.
Timu za Afrika mara nyingi huona ni rahisi kusafiri kwenda kucheza mechi zao kupitia Ulaya. Afrika Kusini,itakua mwenyeji wa kwanza wa kombe la dunia kubidi kushiriki katika kinyan’ganyiro cha kuania nafasi za kombe la dunia tangu pale Itali kufanya hivyo,1934.Ingawa Bafana bafana wanaingia kombe la dunia bila kupingwa, lakini ni njia pekee ya kuwapatia tiketi ya kombe la Afrika la mataifa mwaka huio wa 2010.
Timu 48 za kanda ya afrika zilizosalia katika kinyan’ganyiro hiki zitagaweanywa makundi 12 ya timu 4-4.Washindi na timu 8 bora zilizomaliza nafasi ya pili zinaingia awamu ya pili baada ya Oktoba itakayochezwa kwa mfumo wa ligi.
Halafu timu 20 za mwisho zitagawanywa makundi 5 na kutoka kila kundi mshindi wa kwanza anashiriki katika kombe la dunia.Timu 3 za usoni kila kundi,anajiunga na mwenyeji Angola kwa kombe la Afrika la mataifa 2010 huko Angola.Afrika kusini kwahivyo, inaania tiketi hiyo.
Nahodhja wa mabingwa wa Ulaya AC Milan, Paolo Maldini, ameelezea matumaini kwamba Ronaldo wa Brazil,atakuwa fit karibuni pale AC milan itakapoingia uwanjani alhamisi hii ijayo huko Tokyo,Japan kwa kombe la dunia la klabu bingwa.
AC Milan na Boca Juniors ya Argentina, zinashiriki katika kombe hilo kutoka hatua ya nusu-finali.Kombe hili la dunia lilipangwa kuanza ijumaa kati ya Sepahan ya Iran na Waitakere United ya NZ.Maldini,amekanusha uvumi kwamba anapanga kustaafu baada ya kombe hili la dunia la klabu bingwa huko Tokyo.
Bayern Munich viongozi wa Bundesliga-Ligi ya Ujerumani, wameingia uwanjani jioni hii Allianz arena na chipukizi Duisburg.Munich wanaongoza Ligi hii kwa pointi 1 tu wakiandamwa nyuma na werder Bremen na Hamburg.Hamburg ina miadi leo nyumbani na Cottbus wakati Bremen inabidi kuitembelea Hannover .
Jumapili, mapambano 2 yatakamilisha duru hii:Bayer Leverkusen iliokata tiketi yake ya duru ijayo ya kombe la ulaya la UEFA, itacheza na Hansa Rostock wakati Nüremberg ina miadi na Hertha Berlin.
Kipa wa Bayern Münich, Oliver Kahn amemshauri mpinzani wake wa zamani katika lango la timu ya taifa Jens Lehmann kuiacha mkono klabu yake ya Arsenal London ikiwa anataka kubakia kipa wa Ujerumani katika kombe lijalo la Ulaya 2008.Katika kombe lililopita la dunia, Lehmann aliteuliwa yeye kulinda lango la Ujerumani badala ya Kahn.Hii ikazusha mfarakano kati yao.Kahn alistaafu baada ya kombe la dunia kuichezea timu ya taifa.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger,amekuwa hamchezeshi Lehmann langoni akimpendekeza zaidi Manuel Almunia.Wlfsburg-klabu ya Bundesliga,ikivuma karibuni kutaka kumuajiri Lehmann kulinda lango lao.
Katika Premier League-ligi ya Uingereza ,Chelsea,Manchester United na hata Liverpool zimepania zote kupunguza mwanya usoni kati yao na viongozi wa Ligi Arsenal .Kwani, kabla kulia leo firimbi kwa duru hii, Arsenal ilikuwa bado na mwanya wa pointi 4 na wao hawsatarudi uwanjani kabla ya kesho jumapili.Wnaweza lakini wakagundua mwanya wao huo umezibwa hadi pointi 1 tu kama ilivyo kwa Bayern Munich katika Bundesliga.
Arsenal wana miadi kesho na Middlesbrough.Manchester United wana mteremko leo kwa Derby County yenye kuburura mkia wa Premier League na si hirimu kabisa wa Manchester.
Manchester City wao watakuwa uwnjani kesho kutimiza miadi yao walioweka na Tottenham Hotspurs.Kesho pia aston Villa ilioanza kupata nafuu inaikaribisha Portsmouth wakati Blackburn Rovers wanawakaribisha nyumbani West ham .Bolton Wanderous wanakabili kesho vishindo vya Wigan Athletic.
Katika mpapurano mwengine wa Premier League, Fulham inaonana na Everton wakati Newcastle inavuma nyumbani mbele ya Birmingham.