1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Afrika:Ghana na Namibia

23 Januari 2008

Hatima ya Namibia katika kombe la Afrika inaamuliwa leo.Baada ya kuzabwa mabao 5-1 na Morocco lazima ishinde .

https://p.dw.com/p/Cwg8

Leo ni zamu ya Bafana Bafana-Afrika Kusini na Angola kuteremka uwanjani huko Tamale,katika kombe la afrika la mataifa.

Timu zote 2 zataka kutoa ishara mambo yatakuaje nyumbani miaka 2 kutoka sasa 2010.Angola itakuia mwenyeji wa kombe la Afrika la mataifa na Afrika kusini wa kombe la dunia –la kwanza barani Afrika.

Mpambano wapili leo ni kati ya mabingwa wa 2004-Tunesia na simba wa Terange-Senegal. Hadi sasa, timu za Afrika ya kaskazini zimetamba mbele ya zile za kusini mwa Jangwa la sahara:Mabingwa Misri waliwan’goa meno jana simba wa nyika Kamerun na simba wa Atlas -Morocco wakawameza wanamibia.Je, leo ni zamu ya tai wa Tunisia kutua juu ya kichwa cha simba wa Terange ?

Ghana,Mali,morocco,Ivory Coast na jana Misri na Chipolopolo Zambia,zimeanza vyema katika kombe hili la Afrika: Wakati baadhi ya timu za Afrika magharibi chungu cha juju –wachawi wa dimba chatokota, Senegal inamuachia kila kitu Mwenyenzi Mungu. Huko Maraabu –nde mchawi wao na wakati senegal ikiongozwa hivi punde na El hadji Diouf, Sheikh wao maarufu Mbamba anaomba dua kwamba huu uwe mwaka wa simba wa Terange na hasa baada ya simba wa nyika kuteleza jana mbele ya mafiraouni wa Misri.

Senegal imekaribisha tena mshambulizi wao El hadji doiuf kutoka Bolton Wanderes ya Uingereza kuongoza hujuma zao kama 2002 walipotamba katika kombe la dunia huko Korea ya kusini na Japan na kufululiza njia yao hadi robo-finali –kituo ilipofika kameroun, Itali,1990.

Kinyume lakini na Kameroun-mabingwa mara 4 wa Afrika, Senegal haikuvaa bado taji la Afrika.Huu waomba wanazouni na Maarabu mjini Dakar, ni mwaka wa simba wa Terange.

Rais wao Abdoulaye Wade,ametoa ndege yake binafsi ya rais kuwasafirisha mashabiki hadi Ghana na anatazamia kuwarudisha na kombe Februari 1o.

Tunesia,mabingwa wa afrika 2004 nyumbani wana ajenda nyengine.Wao hawatapenda leo kuvunja rekodi ilioanzishwa na Morocco ,ikafutwa na Misri ya kutamba kwa timu za Afrika ya kaskazini.Isitoshe, wanataka nao kurudia ushindi wao wa 2004 wakiongozwa na kocha wao mfaransa-Roger Lemerre.Lemerre aliiongoza Ufransa kutwaa kombe la Ulaya na sasa anataka kuongeza tena kombe la afrika kikapuni mwake.

Ufunguo wsa ushindi wa Tunesia leo anao Amine Chermiti,kwani ni yeye aliepachika mwaka jana mabao 8 yalioipatia etoile du sahel,kombe la klabu bingwa barani afrika.

Angola baadae ina miadi na Bafana Bafana.kocha wao Mbrazil,Carlos Parreira,amechagua chipuklizi kukusanya maarifa kwa kombe la dunia 2010.Hatahivyo, hatakubali kuvunjiwa hadhi na Angola,na hasa nchini Ghana, nchi alikoanzia kazi yake ukocha na kuisindikiza Ghana hadi finali ya Kombe la Afrika.

Sitapenda mimi kuagua nani ataondoka leo mshindi-Bafana bafana au paa wa Angola.