1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA AFRIKA LA MATAIFA LAPIGA HODI TUNISIA:

15 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CHab
WENYEJI TUNISIA WAPIGIWA UPATU KUWAVUA TAJI SIMBA WA NYIKA KAMERUN TUNAUKAGUA UAUMUZI WA FIFA WA KUREGEZA SHERIA ZA URAIA NA VIPI UTANUFAISHA TIMU KADHAA KATIKA KOMBE HILO

Kombe la Afrika la Mataifa litafunguliwa mjini Tunis, januari 24 kwa changamoto baina ya wenyeji Tunisia na chipukizi Rwanda: Uamuzi wa FIFA-shirikisho la dimba , yamkini ikakuza daraja ya dimba la Afrika . Stadi wa zamani wa klabu ya Arsenal London ya Uingereza na Paris St.Germain ya Ufaransa Kaba Diawara ni mchezaji wa hivi punde alievaa zamani jazi ya timu ya taifa ya Ufaransa na sasa ataichezea Guinea katika Kombe hili.Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 27 aliwahi kuichezea timu ya vijana ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 21. Kuanzia Januari mosi, mwaka huu wachezaji wenye uraia wa nchi mbili na wasiozichezea timu za taifa juu ya umri wa miaka 21 wameruhusiwa kubadili uraia na kuzichezea timu za taifa jengine.Siku za mbele wachezaji watapaswa wasivuke umri wa miaka 21 wakitaka kubadili uraia. FIFA imeshatoa ruhusa kwa Frederic Kanoute kuichezea Mali na Mohammed Lamine Sissoko kuichezea Senegal.Samir Beloufa,Abdfelnasser Oudah na Antara Yahia watavaa jazi ya Algeria katika kombe hili huko Tunisia.

Imetambulika kwamba tangu miaka ya 1960 mamia ya vijana wa afrika wamepotezwa na timu zao za taifa ama kwa kuhamia au kuzaliwa Ulaya ambako wazazi wao walikuja kutafuta maisha bora. Sasa lakini nchi za kiafrika zinavuna matunda ya dim,ba lao. Algeria, inajaribu kumsahjawishi beki mashuhuri wa klabu ya Bundesliga- B.Dortmund Ahmed Madouni,Camel Meriem wa Marseille na Mourad Meghni wa Bologna,Itali kujitayarisha baadae mwaka huu kuichezea Algeria.
Togo nayo inatazamiwa kumshawishi Kodjo Afanou aliekua akiichezea Bordeau na sasa mabingwa wa Asia Al Ain ya Umoja wa Falme za kiarabu kuwasaidia katika kampeni ya kuania tikiti ya Kombe lijalo la dunia.

Simba wa nyika Kamerun yamkini wakamrandia Vincent Pericard wa Portsmouth.Mlinzi wa Liverpool ya Uingereza Djimi Traore alishawishiwa hapo mwanzo na Mali kuichezea timu ya taifa.
Nigeria nayo yamkini ikawataka akina Shola Ameobi alieichezea timu ya chipukizi ya umri wa miaka 21 ya Uingereza au Joseph Dayo Oshadogan alieichezea timu ya vijana ya Itali.

Peggyx Lukunku aliezaliwa Kinshasa lakini mchezaji wa timu chipukizi ya taifa ya Ufaransa ameukataa< mualiko kama huo wa kuichezea Kongo huko Tunisia mwezi huu sawa na Edouard Cisse wa Monaco,aliekua akiichezea West ham ya Uingereza. Alitakiwa Cisse na Senegal lakini alisema la. ·

Tunisia inapigiwa upatu ndio itakayowika nyumbani.Mabingwa watetezi simba wa nyika-kamerun bila shaka watabisha.Tunisia ni miongoni mwa timu zilizojiandaa vyema kabisa kwa changamoto hii na ndio inayofungua dimba na Rwanda -chipukizi wa Afrika ya kati walioitimua nje Black Stars Ghana.Rwanda inaahidi kufa nya maajabu mengine siku hiyo ya ufunguzi sawa na yxale Senegal ilifanya siku ya ufunguzi wa Kombe lililopita la dunia ilipoitimua nje mabingwa Ufaransa.

Hatahivyo, mcheza kwsao hutunzwa, alao huo ndio usemi na Tunisia ikilitimbuga dimba nyumbani ina mashabiki wenye wazimu mkubwa wa mpira.Tunisia inafunzwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Roger Lemerre na ilikua chini ya uongozi wake,Senegal ilipoichezesha Ufaransa kindumbwe-ndumbwe na kuipiga kumbo nje ya Kombe la dunia.Kwahivyo, ukiumwa na nyonka ukiona un'gongo -mara hii rwanda lazima usituke siku ya ufunguzi wa africa Cup.
Kundi A linalojumuisha tunisia,Rwanda,jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Guinea ndilo hafifu kuliko yote ya timu 16.Kocha wa Rwanda Mserbia Ratomir Djukovic hatahivyo haweeki ndoto na anasema ikiwa Rwanda haina matumaini ya kurejea Kigali na kombe la Afrika la mataifa yatosha tu kujipatia maarifa zaidi ya dimba.

Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo- chui wa Zaire waliogeuka simba,wanagombea Kombe hili kwa mara ya 7 katika finali na tangu walipolitwaa 1974 mjini cairo wakiwa njiani kuja katika kombe la dunia hapa Ujerumani, nafasi yao bora kabisa ilikua 1998 walipomaliza nafasi ya tatu huko Burkina faso.Mara hii bila shaka watamkosa stadi wao Shabani Nonda anaeichezea klabu ya Ufaransa ya Monaco.Nonda kitambo sasa ameumia.Maandalio ya simba wa Kinshasa hayakuwa mazuri chini ya kocha wao muingereza Mick Wadsworth.Kikubwa simba wa Kongo waweza kutarajia Tunisia ni kuilaza guinea na rwanda na kuweka ahadi ya kukumbana na Senegal katika robo-finali.

Guinea pia haikujiandaa vyema chini ya kocha Michael Dussuyer lakini ina mastadi kadhaa kama vile Sambegou Bangoura,Titi camara na souleymane Youla. Shabaha ya Guinea ni kukata tikiti ya duru ya pili pengine nyuma ya Tunisia na hivyo changamoto yao ya kwanza dhidi ya simba wa Kongo itakua muhimu kwao.
Kikosi cha Nigeria kwa kombe hili la Afrika kinajumuisha mastadi wengi wa ile timu iliomaliza nafasi ya 3 katika kombe lililopita miaka 2 nyuma nchini Mali.Listi ya Nigeriainajumuisha J,J.Okocha licha ya hofu za hapo kabla kwamba asingeenda Tunisia.Okocha alisema angehiyari kubakia uingereza kuchuma fedha na klabu yake ya Bolton Wonderes kwavile akiba yake alioiweka katika Banki moja ya Nigeria iko hatarini.

Banki hiy imekumbwa na matatizo na okocha nahofia kupoteza fedha zake alizoweka huko.baadae alishawishiwa na chama cha mpira cha Nigeria kujiunga na kikosi kwenda Tunisia.
Pamoja nae ni mastadi wengine kama vile Nwanko Kanu wa Arsenal London,Viktor Agali wa klabu ya Bundesliga Schalke 04 na miongoni mwa wale wanaocheza kwa mara ya kwanza katika Kombe hili la Afrika ni nahodha wa klabu bingwa ya Afrika Enyimba-Romanus Orjinta. Kombe la Afrika la mataifa litaanza januari 24 na kumalizika Februari 14 na linatangulia Kombe sawa na hilo la ulaya la mataifa nchini Ureno hapo Juni.