1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kofi Annan kusimamia usuluhishi Kenya

11 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Co0l

NAIROBI

Marekani imekaribisha uteuzi wa jopo la marais wa zamani watakaongozwa na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa kuchukua nafasi ya upatanishi katika mzozo wa kisiasa nchini Kenya.Juhudi za kutafuta mwafaka wa kisiasa zilizosimamiwa na rais wa Ghana ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika John Kufour zilishindwa kufaulu hapo jana baada ya pande zote mbili upinzani na serikali kushikilia misimamo yao.

Viongozi hao wawili rais Mwai Kibaki na mpinzani wake Raila Odinga wako katika mvutano mkubwa wa kisiasa kufuatia matokeo ya uchaguzi wa rais yanayotiliwa shaka yaliyompa ushindi bwana Kibaki.Hata hivyo rais Kufour amesema pande zote mbili zimekubali kushiriki mazungumzo yatakayoongozwa na Kofi Annan.Kiasi cha watu 600 waliuwawa katika machafuko yaliyoibuka kufuatia uchaguzi wa tarehe 27 maelfu ya wengine wameachwa bila makaazi.