1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Koeman kuifunza Uholanzi baada ya Kombe la Dunia

6 Aprili 2022

Kocha wa zamani wa Barcelona Ronald Koeman atachukua mikoba ya ukocha wa timu ya taifa ya Uholanzi kutoka kwa Louis van Gaal baada ya Kombe la Dunia. Haya ni kwa mujibu wa Shirikisho la Kandanda la Uholanzi.

https://p.dw.com/p/49XR5
Fußball I Champions League I SL Benfica - FC  Barcelona
Picha: Armando Franca/AP/picture alliance

Mwishoni mwa wiki iliyopita, van Gaal alifichua kwamba amekuwa akipokea matibabu ya saratani ya tezi dume kwa miaka miwili iliyopita ila bado anatarajia kuiongoza timu hiyo katika fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar mwezi Novemba.

Hii itakuwa mara pili kwa Koeman kuwa kocha wa timu hiyo ya taifa baada ya kuwafunza hao "The Orange" kwa mara ya kwanza kati ya 2018-2020 alipoondoka na kuwa kocha wa Barcelona.

Flash-Galerie Bundesliga 2011 Saisonrückblick
Kocha wa Uholanzi kwa sasa Luis van GaalPicha: picture alliance/dpa

Alifutwa kazi na miamba hao wa Uhispania mnamo mwezi Oktoba 2021 baada ya miezi 14 tu ambapo Lionel Messi aliihama klabu hiyo pia na kujiunga na Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Uholanzi watacheza mechi yao ya ufunguzi katika Kombe la Dunia dhidi ya mabingwa wa Afrika Senegal hiyo ikiwa mechi ya kundi A ambalo lina wenyeji Qatar na Ecuador pia.