1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kocha wa Bayern amtetea kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani

Sylvia Mwehozi
15 Oktoba 2020

Kocha wa Bayern Hansi Flick amemtetea bosi wake wa zamani Joachim Loew wakati timu ya taifa ya Ujerumani ikikoselewa vikali na wachezaji wa zamani wa timu hiyo.

https://p.dw.com/p/3jxzo
UEFA Super Cup 2020 Bayern München
Picha: Frank Hoermann/picture-alliance/Sven Simon

"Nadhani kinachotokea kwa sasa tayari kipo juu" Flick alisema siku ya Jumatano." Jogi amefanya kazi ya kupendeza kama kocha wa taifa. "

Meneja huyo wa Bayern alikuwa akizungumza siku moja baada ya timu ya Ujerumani kutoka sare ya mabao 3-3 na Uswisi katika mechi za kuwania kufuzu katika Kombe la Mataifa Barani Ulaya au UEFA Nations League, huku kiwango chake katika nafasi ya ulinzi hasa kikizungumzwa mno.

Kocha huyo wa Bayern alikuwa msaidizi wa Loew wakati Ujerumani iliposhinda kombe la dunia la mwaka 2014 na aliwakosoa baadhi ya wachambuzi ambao alisema "hawajakuwa na mpira miguuni mwao kwa miaka 25 au 30".

Alikumbuka pia wale wataalam sasa wanaoingia kutoka nje walijibu vibaya kwa maoni kama hayo wakati walipokuwa wakicheza. "sasa wako pembeni na wanatoa jambo moja au jingine, "Flick alisema." Hali hii haifanyi Soka la Ujerumani au hali kuwa nzuri. "

Miongoni mwa wachezaji wa zamani ambao wamekuwa na ukosoaji ni, Lothar Matthaeus, Dietmar Hamann, Olaf Thon, Bastian, Schweinsteiger na Berti Vogts.