1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kocha Van Gaal afichua kuwa anaugua saratani ya tezi dume

4 Aprili 2022

Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis van Gaal amefichua kuwa anaugua saratani ya tezi dume lakini bado anapanga kuiongoza timu hiyo katika Kombe la Dunia nchini Qatar Novemba mwaka huu

https://p.dw.com/p/49RoJ
Großbritannien London | Louis van Gaal
Picha: Adam Davy/empics/picture alliance

Van Gaal amesema hata wachezaji wake katika kikosi cha taifa hawakujua kuhusu ugojwa wake huo hata ingawa alikuwa akipokea matibabu saa za usiku wakati akiwa kwenye kambi za mazoezi na timu yake. "Ni sehemu ya Maisha, nimepitia mengi sana ya ugonjwa na kifo, katika familia yangu mwenyewe, mke wangu.” Alisema. Van Gaal mwenye umri wa miaka 70 alimpoteza mke wake wa kwanza kupitia saratani.  

Van Gaal anaifundisha timu ya taifa ya Uholanzi kwa mara yake ya tatu. Aliiongoza timu hiyo hadi nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014. Pia alizifundisha klabu za Barcelona, Manchester United, Bayern Munich na Ajax, na kubeba Kombe la Ulaya mwaka wa 1995 akiwa na klabu hiyo ya Amsterdam.

Uholanzi imepangwa katika kundi moja na wenyeji Qatar, Senegal na Equador katika Kombe la Dunia.

afp