1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kocha Flick awataka wachezaji kujituma kabla ya Euro 2024

12 Juni 2023

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Hansi Flick amesisitiza kuwa wachezaji wake lazima wawe tayari kufikia upeo wao na kujituma zaidi ili kuwa na mchango mzuri katika mashindano ya Ulaya mwaka ujao nchini Ujerumani

https://p.dw.com/p/4STak
Fußball | Bayern München - Paris Saint-Germain | Hansi Flick
Picha: Sven Hoppe/dpa/picture alliance

Flick amesema hakufurahishwa na tabia na kujitolea kwa beki Niklas Süle na ndio sababu amemuwacha nje ya kikosi kitakachocheza mechi za leo jioni dhidi ya Ukraine, Ijumaa nchini Poland na Juni 20 dhidi ya Colombia. "Tunacheza mfumo mpya. Sio rahisi kwa wachezaji na bila shaka pia wao wako katika hali ambayo kwa sehemu wako likizinoni na kwa sehemu katika mazingira tofauti, mazingira ya kuwa fit. Na nimewaambia wachezaji kutarajia hilo bila shaka, jinsi ya kujituma na kuumia kiasi hata mjini Bremen katika mechi ya leo kwa hiyo kwetu sisi kila mechi ya kimataifa ni ya kutusaidia kupata kikosi chetu cha wachezaji 11 watakaoanza mashindano ya Juni 14 mwaka ujao"

Wakati wa mechi ya leo ya kirafikidhidi ya Ukraine, wachezaji wa Ujerumani watavaa jezi maalum zilizotengeneza kuadhimisha mchezo wa 1,000 wa timu ya taifa. Na baada ya kipenga cha mwisho, jezi hizo zitapigwa mnada na shirikisho la soka Ujerumani – DFB ambapo fedha zitakazokusanywa zitatolewa kama msaada kwa Ukraine.

Ujerumani wamefuzu moja kwa moja kama wenyeji wa Euros 2024 na kwa hiyo wanacheza tu mechi za kirafiki hadi mashindano hayo.

Nations League

Tukibaki na kandanda la Ulaya, Croatia huenda ikahitimisha msimu wake wa kufana Zaidi kwa ushindi katiki fainali za wiki hii za Ligi ya Mataifa ya UEFA dhidi ya wapinzani watatu wanaolenga kurejesha ubora wao uliopotea mwishoni mwa kampeni ndefu.

Kinyang'anyiro hicho cha timu nne kinaandaliwa Uholanzi wiki hii ambapo Croatia waliofika fainali ya Kombe la Dunia watakabana koo na wenyeji katika nusu fainali ya kwanza mjini Rotterdam Jumatano kabla ya Italia na Uhispania kukuzana saa 24 baadae mjini Enschede. Washindi watatinga fainali mjini Rotterdam Jumapili, ambayo itachezwa baada ya kujulikana mshindi wa nafasi ya tatu.

dpa, afp