Wakfu wa Mo Ibrahim, kwa mara nyingine tena umeshindwa kumpata mshindi wa tuzo ya uongozi bora barani Afrika kwa mwaka 2016. Wakfu huo ulitangaza kuwa hakuna kiongozi wa zamani wa Afrika aliyekidhi vigezo vya kupewa tuzo hiyo inayoambatana na kitita cha Dola milioni tano. Aidha, wanasiasa wengi ni wazee na vijana hawapewi nafasi za kushiriki siasa na uchumi. Mada katika kipindi cha Maoni.