1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiwanda cha mafuta Urusi chashambuliwa kwa droni

13 Machi 2024

Mashambulizi ya droni yaliyolenga kiwanda cha kusafisha mafuta katika eneo la Kusini Mashariki mwa Urusi la Ryazan yamesababisha moto na watu chungunzima wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4dSaA
 Eneo la Kusini Mashariki mwa Urusi la Ryazan
Eneo la Kusini Mashariki mwa Urusi la RyazanPicha: Mikhail Metzel/TASS/dpa/picture alliance

Mashambulizi ya droni yaliyolenga kiwanda cha kusafisha mafuta katika eneo la Kusini Mashariki mwa Urusi la Ryazan yamesababisha moto na watu chungunzima wamejeruhiwa.

Gavana wa Ryazan, Pavel Malkov amefahamisha kupitia ujumbe alioandika kwenye mtandao wa Telegram, kwamba kiwanda hicho cha mafuta cha Ryazan kilishambuliwa kwa droni na watu wamejeruhiwa.

Rais Vladmir Putin amesema Ukraine inaongeza mashambulizi dhidi ya maeneo ya Urusiili kuvuruga uchaguzi ujao wa rais.

Wiki hii Urusi imekabiliwa na mashambulizi makubwa kadhaa ambayo hayajawahi kuonekana tangu ilipopeleka wanajeshi wake katika vita nchini Ukraine zaidi ya miaka miwili iliyopita. Viwanda chungunzima vya mafuta vimelengwa katika wimbi  la mashambulizi ya droni.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW