1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kituo cha kuwahudumiwa walazimishwao ndoa

Hamidou, Oumilkheir4 Januari 2013

Mjini Berlin kuna kituo kinachowahudumia wanawake wenye asili ya kigeni ambao kutokana na mivutano pamoja na familia zao, kama vile kulazimishwa kuolewa, wanalazimika kukimbia nyumbani na kutafuta hifadhi nje ya familia.

https://p.dw.com/p/17Dec

Oummilkheir analiangazia shirika la Papatya linalowashughulikia zaidi wasichana kutoka Uturuki, Kurdistan na katika zile nchi za Kiarabu ambako matumizi ya nguvu yanaangaliwa kama njia pekee ya kuitakasa hadhi ya familia. Kituo hiki kipo pia Ufaransa, ambako kinawashughulikia wasichana wenye asili ya Afrika Kaskazini na Uingereza kinakowahudumia wasichana wenye asili ya Pakistan.