1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kisiwa cha Mayotte chawa rasmi sehemu ya Ufaransa

1 Aprili 2011

Kisiwa cha Mayotte kimejiunga rasmi hii leo kuwa sehemu ya nchi ya Ufaransa. Hatua hii inafuatia baada ya wananchi wa kisiwa hicho kupiga kura ya maoni iliyoandaliwa na Ufaransa kuhusu kujitenga na Comoro.

https://p.dw.com/p/10lUo
--- DW-Grafik: Peter Steinmetz 2011_03_25-Komoren-Mayotte.psd
Visiwa vya ComoroPicha: DW

Hata hivyo utawala wa serikali kuu ya Comoro huko Moroni una msimamo mwengine kuhusu hatua hiyo.Ili kujua zaidi kuhusu vipi suala hili lilivyopokelewa na serikali,Saumu Mmwasimba amezungumza na mkuu wa kamati ya Komoro inayohusika na suala la kisiwa cha Mayotte na balozi wa Komoro nchini Afrika Kusini Ahmed Thabit.

Mwandishi: Saumu Mwasimba Mhariri: Josephat Charo