1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Kishida aahidi kuimarisha jeshi la Japan

23 Januari 2023

Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida amesema leo kuwa nchi hiyo inakabiliwa na mazingira magumu kabisa ya usalama katika kanda hiyo tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

https://p.dw.com/p/4MZjM
Japan | Parlament | Premierminister Fumio Kishida
Picha: YUICHI YAMAZAKI/AFP/Getty Images

Waziri Mkuu Kishida ameahidi kuongeza idadi ya jeshi lake chini ya mkakati mpya wa usalama, pamoja na kupambana na idadi inayopugua kwa kasi ya watoto wanaozaliwa ili nchi hiyo iweze kudumisha nguvu ya taifa. 

Katika hotuba yake ya sera ya nchi wakati akifungua kikao cha bunge, Kishida amesema diplomasia hai inapaswa kupewa kipaumbele, lakini inahitaji kile alichokiita nguvu ya ulinzi ili kwenda sambamba.

Mkakati mpya wa usalama wa Japan unalenga kuyadhibiti malengo ya China ya kudai maeneo ya mipaka.