1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kipindupindu chaathiri watu 2,786 katika kambi ya Daadab

30 Mei 2023

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka MSF limesema mamia ya wakimbizi katika kambi za Dadaab nchini Kenya wameathiriwa na mripuko wa ugonjwa kipindupindu.

https://p.dw.com/p/4Rypz
DW Akademie | Straße in Kakuma in Kenia
Picha: Laura Wagenknecht/DW

Taarifa ya shirika hilo inasema takribani watu 2,786 wameathirika hadi wakati huu, na kuongeza kuwa hali hiyo inasweza kuchangia hatari ya kusababisha miripuko mingine ya magonjwa ya tumbo.  Hayo yanaripotiwa katika kipindi ambacho idadi ya watu katika kambi hiyo ikiongezeka kwa kasi.

Kambi za Dadaab ni makazi ya watu zaidi ya 300,000 na tatizo la ukame katika nchi jirani ya Somalia, idadi watu inaongezeka, hali ambayo imeathiri huduma za upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira.