Kwa mara nyengine tena, Marekani na Iran zimo kwenye vita vya maneno, ambavyo vinaelekea kuwa vita vya silaha sasa, ingawa wengi wanasema hakuna upande wowote ulio tayari kwa mapigano. Wakati jitihada za mataifa kama vile Ujerumani, Oman na Iraq zikiendelea muda huu kuzuwia uwezekano wa vita vyengine kwenye Ghuba hiyo ya Uajemi, Maoni Mbele ya Meza ya Duara hivi leo inaitathmini hali ya mambo ilivyo. Je, kipi hasa kinachochea hali hii ya kutishiana baina ya wababe wawili mahasimu wa kihistoria?
Je, kwa namna gani siasa ya nje ya Marekani imesalia kuwa ile ile kuelekea Iran miaka nenda miaka rudi, licha ya tawala kubadilika mara kwa mara?
Je, Iran nayo ni mkoswaji mnyonge tu kwenye mzozo huu, au ni mchokozi kweli anayepaswa kukomeshwa - kwa maneno ya John Bolton - mshauri wa usalama wa rais wa Marekani, Donald Trump?
Na kubwa kuliko yote, kuna uwezekano wa kupatikana amani ya kweli ya kudumu kwenye Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika wakati ambapo Marekani na Iran zinatazamana zinavyotazamana sasa?
Mwongozaji wa meza ya duara: Mhammed Khelef - Bonn, Ujrumani
Wataalamu katika meza ya duara
Nicolas Boaz - Profesa na mtaalamu wa siasa za kimataifa,Washington, D.C. Marekani
Abdulfattah Musa - Mwandishi habari na mchambuzi, Tehran, Iran
Ahmed Rajab- Mwandishi habari na mchambuzi wa masuala ya kimataifa, London, Uingereza
Mohamed Issa - Mchambuzi wa masuala ya kimataifa, Dar es Salaam, Tanzania