1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Puigdemont atoa sharti la kuinusuru serikali ya Uhispania

5 Septemba 2023

Kiongozi wa zamani wa Catalonia Uhispania Carles Puigdemont amesema chama chake kitashiriki mazungumzo ya kuiwezesha serikali kubakia madarakani iwapo watu waliongoza harakati za kujitenga kwa Catalonia watapewa msamaha.

https://p.dw.com/p/4Vz9g
Belgien EU-Gipfels l Carles Puigdemont im Europäischen Parlament
Picha: Dwi Anoraganingrum/Geisler-Fotopress/picture alliance

Mwanasiasa huyo aliyekimbilia uhamishino muda mfupi baada ya kuendesha kura ya maoni ya uhuru wa Catalonia mwaka 2017, ametoa sharti hilo alipozungumza na waandishi habari mjini Brussels.

Amesema pindi wanaharakati wenzake wa uhuru wa Catalonia watapewa msamaha wa tuhuma zinazohusiana na kura ya maoni ya uhuru chama chake cha Junts kitakuwa tayari kushiriki mazungumzo na chama cha mrengo wa shoto cha waziri mkuu Pedro Sanchez. 

Puigdemont aitaka serikali Uhispania kuheshimu demokrasia

Sanchez anahitaji uungaji mkono wa vyama vidogo vya majimbo ikiwemo cha Puigdemont ili abakie madarakani baada ya matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwezi Julai kutotoa mshindi wa wazi