1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Kiongozi wa RSF nchini Sudan akutana na rais wa Kenya

3 Januari 2024

Kiongozi wa kikosi cha wanamgambo nchini Sudan cha RSF Mohamed Hamdan Daglo amefanya mazungumzo na rais wa Kenya William Ruto, ikiwa ni juhudi za kikanda ili kujaribu kusitisha vita kati ya RSF na jeshi la Sudan.

https://p.dw.com/p/4apo1
Sudan | Mohamed Hamdan Daglo
Kiongozi wa kikosi cha wanamgambo nchini Sudan cha RSF Mohamed Hamdan DagloPicha: Ashraf Shazly/AFP

Ruto amesema anathamini nia ya RSF na Daglo ya kutaka kuumaliza mzozo huo kwa njia ya mazungumzo, na kwamba mchakato wa amani unaoendelea chini ya usimamizi wa Jumuiya ya maendeleo Afrika Mashariki na pembe ya Afrika IGAD, unapaswa kufikia suluhu ya kisiasa itakayoleta amani ya kudumu nchini Sudan.

Kulingana na makadirio, vita hivyo nchini Sudan vilivyoanza mwezi Aprili mwaka jana, tayari vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 12,000 huku Umoja wa Mataifa ukisema kuwa zaidi ya watu milioni 7 wameyakimbia makazi yao.