1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa RSF amefanya ziara ya kikanda

1 Januari 2024

Kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa mapigano yaliyodumu kwa zaidi za miezi minane, baina ya jeshi la Sudan na kundi la wanamgambo la RSF kiongizi wa kundi hilo afanya ziara nje ya Sudan.

https://p.dw.com/p/4akfm
Sudan | Mohamed Hamdan Daglo
Picha: Ashraf Shazly/AFP

Kiongozi wa kundi hilo Mohamed Hamdan Daglo amefanya ziara ya kikanda nje ya taifa hilo ambapo amezitembelea Djibout, Ethiopia pamoja na Uganda. Ziara ya kiongozi huyo imekuja wakati ambao, wanadiplomasia mbalimbali wapo katika juhudi za mazungumzo baina yake, mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan. Majenerali hao wanaohasimiana hawajawahi kukutana ana kwa ana, tangu kuzuka kwa mzozo nchini humo, uliopelekea vifo vya watu zaidi ya 12,000 na mamilionikuyahama makazi yao.Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X zamani Twitter, Daglo ameandika kuwa, alizungumza na Rais wa Djibout Ismail omar Guelleh, na kumueleza dhamira yao ya kutaka kumaliza mzozo huo ulipelekea mateso kwa watu wa Sudan.