1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa Libya asisitiza kuundwa serikali moja ya Afrika

15 Desemba 2010

Anaungwa mkono na rais wa Senegal, Abdoulaye Wade

https://p.dw.com/p/QaR8
Kiongozi wa Libya, Moammar GadhafiPicha: AP

Kiongozi wa Libya Kanali Moammar Gadhafi akiungwa mkono na Rais Abdoulaye Wade wa Senegal amesisitiza tena kuhusu ndoto yake ya kuwa na serikali moja ya Afrika na kutoa wito wa kuwepo kwa jeshi moja la bara hilo.

Akizungumza katika sherehe za kuyakinisha uafrika na utamaduni wake nchini Senegal, ameliezea bara hilo kuwa ni mawindo ambayo mbwa mwitu wote duniani wanataka kuwinda, kwa kuufanyia ukiritimba mali ghafi ya bara hilo kama vile madini au samaki.

Amesema ili kuupiga vita ukoloni mamboleo,ni lazima bara la Afrika liungane.Kwa upande wake Rais Wade wa Senegal amesema kuwepo kwa serikali moja ya kiafrika ndiyo suluhisho pekee la kuwakomboa watu wa bara hilo na kulifanya liheshimike kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.

Viongozi wengine waliyoudhuria sherehe hizo ni pamoja na Rais Malam Bacai Sanha wa Guinea-Bissau, Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia na Pedro Pires wa Cape Verde.