1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Tiani asema Niger inaelekea kupata "uhuru kamili"

26 Julai 2024

Kiongozi wa kijeshi nchini Niger Abdourahamane Tiani amesema nchi hiyo inaelekea kupata kile alichokiita "uhuru kamili" wakati akitoa hotuba ya kuadhimisha mwaka mmoja wa mapinduzi yaliyomuingiza madarakani.

https://p.dw.com/p/4ikZJ
Kiongozi wa kijeshi nchini Niger Abdourahamane Tiani
Kiongozi wa kijeshi nchini Niger Abdourahamane Tiani Picha: ORTN/Télé Sahel/AFP/Getty Images

Tiani ameeleza kuwa safari ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi kupata uhuru kamili haizuiliki, siku mbili tu baada ya Ufaransa ambayo ni koloni la zamani la Niger, kutaka aliyekuwa rais Mohamed Bazoum aachiliwe huru mara moja na bila masharti kutoka kizuizini.

Katika hotuba aliyoitoa kupitia televisheni ya taifa, kiongozi huyo wa kijeshi amesema hakuna serikali wala shirika lolote litakalotoa maagizo ya jinsi nchi hiyo inavyopaswa kuendeshwa.

Soma pia: Wanajeshi 47 wauawa katika shambulio la kigaidi Niger

Abdourahamane Tiani aliingia madarakani mnamo Julai 26, mwaka uliopita baada ya kumpindua rais Mohamed Bazoum. Tiani alihudumu kama mkuu wa kitengo cha ulinzi wa rais kabla ya hatimaye kumuondoa madarakani.

Tangu ulipoingia madarakani, utawala huo wa kijeshi umejitenga na Ufaransa na kujenga usuhuba wa karibu na Urusi.