1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Kiongozi wa Hamas ukingo wa Magharibi afariki kizuizini

26 Julai 2024

Kiongozi mmoja wa kundi la Hamas katika ukingo wa Magharibi, Mustafa Muhammad Abu Ara, amefariki akiwa kizuizini Israel baada ya afya yake kuzorota.

https://p.dw.com/p/4ikZA
Wafungwa wa zamani wa Kipalestina walioachiliwa huru na mamlaka ya Israel walipowasili katika mji wa Beitunia, Ukingo wa Magharibi.
Wafungwa wa zamani wa Kipalestina walioachiliwa huru na mamlaka ya Israel walipowasili katika mji wa Beitunia, Ukingo wa Magharibi.Picha: Nasser Nasser/AP/picture alliance

Tume inayohusika na masuala ya wafungwa wa Kipalestina imesema katika taarifa kuwa Muhammad Abu Ara, mwenye umri wa miaka 63 amefariki baada ya kukimbizwa hospitali kutoka jela ya Ramon kusini mwa Israel. 

Tume hiyo imeongeza kabla ya kukamatwa kwake, Muhammad Abu Ara alikuwa na matatizo ya kiafya na alihitaji uangalizi wa karibu wa madaktari lakini kama ilivyo kwa wafungwa wengine, alipitia mateso.

Soma pia: Mashambulizi mapya yatikisa Ukanda wa Gaza 

Kiongozi huyo wa Hamas alikamatwa mnamo mwezi Oktoba mwaka jana na kuzuiwa kupata huduma za matibabu. Hata hivyo, Israel haijatoa kauli yoyote kuhusu kifo chake.

Takriban Wapalestina 18 wamefariki wakiwa kizuizini Israel tangu kuanza kwa mzozo kati ya Hamas na Israel mnamo Oktoba 7.