SiasaMarekani
Kinyang´anyiro cha ´Jumanne Kuu´ chawadia Marekani
5 Machi 2024Matangazo
Rais Joe Biden anayewania muhula wa pili bila upinzani mkubwa kupitia chama cha Democratic anatazamiwa kupata ushindi wa wazi kwenye kura hizo zinazofanyika katika majimbo 16 na eneo jingine moja lililo chini ya milki ya Marekani.
Kwa upande wa Rebuplican, uchaguzi huo wa mchujo unaofahamika pia kama "kinyang´anyiro cha Jumanne Kuu" unatazimiwa kufungua milango zaidi kwa rais wa zamani Donald Trump kuelekea kuteuliwa kuwa mgombea wa urais wa mwezi Novemba.
Tangu kuanza kwa kura za mchujo Trump ameshinda kwenye majimbo yaliyokwishapiga kura huku mpinzani wake aliyebakia Nikki Haley alipata ushindi wa kwanza hapo jana kwenye wilaya ya Washington DC.