1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Watu wengine tisa wagunduliwa na virusi vya Ebola nchini DRC

23 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNU

Shirika la afya duniani WHO limetoa taarifa kwamba watu wengine tisa wameambukizwa virusi vinavyo sababisha ugonjwa wa Ebola katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Takriban watu 174 wamefariki katika jimbo la magharibi la Kasai kufuatia kuzuka tena ugonjwa huo.

Dalili za ugonjwa wa Ebola ambazo ni joto kali mwilini na kuendesha damu ziligunduliwa katika jimbo la Kasai kwa mara ya kwanza tarehe 27 mwezi wa Aprili.

Hadi sasa tiba ya ugonjwa huo bado haijapatikana.

Ugonjwa wa Ebola uliwauwa takriban watu 200 mnamo mwaka 1995 katika eneo la Kikwit lililo kilomita 400 magharibi mwa jimbo la Kasai nchini jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.