1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Rais Kabila amfuta kazi waziri wake wa uchukuzi

5 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7IF

Rais Joseph Kabila wa jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo amemfuta kazi waziri wa uchukuzi bwana Remi Henry Kuseyo Gatanga kufuatia ajali ya ndege iliyosababisha vifo vya watu 38.

Msemaji wa rais bwana Kudura Kasongo amesema kuwa rais Kabila amemfuta kazi waziri huyo kwa kutochukua hatua madhubuti za kusimamia usafiri wa anga nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Abiria 20 waliokuwa ndani ya ndege hiyo na wafanyakazi watatu wote walifariki.

Watu kumi na tano wengine waliuwawa ndege hiyo ilipoanguka kwenye nyumba za watu muda mfupi tu ilipopaa kutoka mwenye uwanja wa kimataifa wa Ndjili.

Takriban watu 30 wamejeruhiwa vibaya kwenye ajali hiyo iliyotokea jana.

Uchunguzi umeanza mara moja kutathmini kilichosababisha ajali ya ndege hiyo aina ya Antonov 26 kutoka Urusi mali ya shirika la ndege la Africa One la nchini Kongo.

Ndege hiyo ilikuwa imekodishwa na kampuni ya Malila na ilikuwa inaelekea kusini mwa jimbo la Kasai.

Wafanyakazi watatu katika ndege hiyo walikuwa raia wa Ukraine.