KINSHASA:Nafasi za kazi za waandamanaji wa MONUC zajazwa
26 Agosti 2007Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Kongo MONUC umejaza nafasi za kazi kwa muda za wafanyikazi wake walioandamana Alhamisi iliyopita kudai nyongeza ya mshahara.Majukumu ya nafasi hizo za kazi yanatimizwa na wafanyikazi wa kimataifa.Mamia ya wafanyikazi wa ujumbe huo wa MONUC waliandamana Alhamisi iliyopita na kusababisha huduma za umeme na matangazo ya redio kusitishwa kwa muda.
Ujumbe wa MONUC unatoa wito kwa wafanyikazi hao wanaoandamana kurejea kazini na kutisha kuwaachisha kazi endapo hawatatimiza hilo.Mazungumzo ya kujadilia suala hiyo yanatarajiwa kuendelea hapo kesho mjini Kinshasa.
Mamia ya wafanyikazi wasio wa kimataifa vilevile vibarua wa kila siku walianzisha maandamano hayo ya kwanza ya aina hiyo kutokea tangu MONUC kuanzishwa mwaka 99.Chanzo cha maandamano hayo ni mkwamo wa majadiliano kuhusu malipo.
Uongozi wa MONUC unaeleza kuwa unataka kupata suluhu ya mkwamo huo ila kusistiza kuwa masuala ya bajeti na utendaji kazi kwa jumla unategemea mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa,.