1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa: Waandamanaji wawili wauawa kwa kupigwa risasi

10 Julai 2020

Waandamanaji wawili wameuawa kwa kupigwa risasi huku polisi mmoja akiuawa pia baada ya kutokea ghasia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

https://p.dw.com/p/3f5rp
Picha ya maktaba
Picha ya maktabaPicha: Getty Images/AFP/A. Mpiana

Ghasia hizo zimechochewa na mipango ya kumteua mwenyekiti mpya wa tume huru ya uchaguzi nchini humo.

Mwili wa mmoja wa waandamanaji waliouawa umepelekwa katika hospitali mjini Lubumbashi, kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo cha Umoja wa mataifa mjini Kinshasa, mauaji hayo yametokea baada ya polisi kutumia risasi kuwatawanya waandamanaji.

Katika purukushani hizo, polisi kadhaa pia wamejeruhiwa.

UN imesema ghasia hizo zimesababisha uharibifu wa mali ikiwemo ofisi za vyama vya kisiasa zilizoshambuliwa na kuchomwa moto.

Maandamano hayo yamechochewa na uamuzi wa bunge la kitaifa kumteua Ronsard Malonda kama mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini humo, CENI.