KINSHASA: Visa ya ubakaji na ukahaba vyachunguzwa na Umoja wa Mataifa
17 Agosti 2006Matangazo
Umoja wa Mataifa unachunguza visa vya ukahaba na ubakaji wa watoto unaowahusisha wanajeshi wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Tume ya amni ya umoja wa Mataifa nchini Kongo imesema uchunguzi huo unajumulisha visa vya watu kuwashawishi wasichana wadogo wakubali kwenda kufanya kazi kama makahaba katika maeneo ya Kivu Kusini, ambako majeshi ya Umoja wa Mataifa yanalinda usalama.
Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Kongo imeapa kuwaadhibu maofisa wake watakaopatikana na hatia katika uchunguzi huo.