KINSHASA: Operesheni ya dharura kupambana na Ebola
13 Septemba 2007Matangazo
Wafanyakazi wa afya wamezindua operesheni ya dharura kupambana na mripuko wa homa ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Shirika la Afya Duniani-WHO limetoa dawa na zana za kinga na zinapelekwa katika maeneo yaliyoathirika.Waziri wa Afya,Victor Makwenge Kaput,ametembelea mji wa Kananga ulio kama kilomita 300 kutoka kijiji cha Kanungu ambacho kimeathirika vibaya zaidi katika eneo la Kasai ya Magharibi.Serikali imesema,tangu mwezi wa Aprili mwaka huu,homa ya Ebola imeua watu 166 kutoka jumla ya wagonjwa 372.